Mwenyekiti
wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza
mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya
chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine
wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni
Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa
chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa
chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia
kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli
Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko
kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka
huu.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa UKAWA,uliofanyika mapema leo jijini Dar
Mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri,Deodatusi Balile akitaka
ufafanusi kuhusiana na umoja huo wa UKAWA kumkaribisha rasmi Mhe.Lowassa
kujiunga na UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika katika makao
makuu ya chama cha CUF jijini Dar
Mmoja
wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo
aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na
umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar
Viongozi wa UKAWA wakiandika maswali waliokuwa wakiulizwa na Wanahabari kwenye mkutano hou uliofanyika jijini Dar
Mwenyekiti
wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza mbele ya
Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama hicho
jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wa wanaounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),ambapo mkutano huo ulizungumzia pia
kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli
Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko
kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka
huu,kulia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia na
kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe pamoja na
Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi (hayupo pichani)
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo
mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya
chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya
kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama
kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji
kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi
wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa
tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano
huo na Wanahabari.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo
mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana makao makuu ya chama cha
CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na
UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa
ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba
ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo)
tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua
ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
Mwenyekiti
wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akipeana mkono na
Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe mara baada ya
kuzungumza na Waaandishi wa Habari makao makuu ya chama cha CUF,mapema
leo mchana jijini Dar,ambapo kwa pamoja kama UKAWA wamemkaribisha rasmi
Mhe.Lowassa kujiunga na umoja huo na kwamba watampa nafasi.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
UMOJA wa katiba ya Wananchi nchini (UKAWA) vinamkribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga katika na umoja huo pamoja na watanzania wengine katika mapambano ya kuindoa CCM madarakani.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi
(CUF), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo,Mwenyekiti wa Taifa wa
NCCR-Mageuzi,James Mbatia amesema
wanawalika watanzania wote kujiunga na UKAWA katika kuweza kuleta
mabadiliko katika kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM)
katika kuweza kusimamia nchi.
Mbatia
amesema kuwa wanamualika Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kutokana
na kuwa mchapakazi na mfuatilialiaji katika majukumu ambayo anayatoa na
uwezo anao katika kusimamia.Amesema
akiingia Lowassa katika umoja huo watashirikiana kwa karibu kutokana
na kutambua kuwa ni mhamasishaji na ni mtu mwenye kuthubutu.
Aidha amesema kuwa watamsimamisha mgombea mmoja katika kila nafasi katika kupeperusha bendera ya UKAWA katika uchuguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 25 mwaka huu.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba amesema tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowassa zinatokana na mfumo uliopo. Amesema
wanatarajia kutaja jina la mgombea Urais Agosti Nne Mwaka huu na
atapatikana kutokana na taraibu zilizowekwa na umoja huo.
Mbatia
hakuweza kuweka wazi kuwa wanamkaribisha Lowassa kujiunga na chama kipi
kutokana na ukawa sio chama kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya
siasa nchini.
Mwenyekiti
wa NLD,Dk.Emmanuel Makaidi amesema Lowassa akigombea Urais atamkubali
na tuhuma zinazomkabili kiongozi zingekuwa za kweli angepelekwa
mahakamani lakini bado yupo na wenye tuhuma wamefikishwa mahakamani .
Katika mkutano wa UKAWA masuali yalilenga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga huko na tuhuma
zake wakati vyama hivyo vilikuwa vikinadi juu ya kutokuwa na usafi na
pamoja na uhusikaji katika tuhuma ya mchakato wa umeme wa dharula
kupitia kampuni ya Richmond.
Comments