MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI LEO, KUFANYA KONGAMANO LA WATOTO NA WAZAZI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM


Na Mwandishi Wetu
MTOTO  mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri  wa kujijengea uwezo wa kujiamini  anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani,  Lonnie Hudson  maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua  jijini Dar es Salaam , leo.
King Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson  ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa  taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.
Kesho mtoto huyo atafanya  kongamano kubwa  la watoto na wazazi  katika Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za  watu ambao wamekata  tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.
“Najisikia furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa. Hususani  kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia zao, kujiamini na  kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,” alisema.
King Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana na kuishia kulaumu  matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya matatizo yao.

“Kila mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na kushangaza watu waliokwenda kumlaki.

Mkurugenzi wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.

“King Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na  kipawa  alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho  Urafiki,  ili waweze kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu kuanzia saa tano asubuhi,”alieleza Henjewele.
King Nahh akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo


 Akikabidhiwa shada la mauwa uwanjani hapo
King Nahh akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanjani hapo
 Meneja wa King Nahh akisisitiza jambo kwa wanahabari

 King Nahh akicheza ngoma ya utamaduni
 King Nahh akizungumza na wananchi katika viunga vya uwanja wa ndege
 Akiwa amepozi na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo

 Akisaini kitabu cha wageni katika Supermarket ya Uchumi
 Akimlisha keki mmoja kati ya wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
 Akilishwa keki na msanii nyota wa filamu, Iluminata Alfonce 'Dotnata'
 Akikabidhiwa 'token' na Meneja wa Uchumi Supermarket kwa ajili ya kununulia bidhaa katika kipindi atakachokuwa nchi, pembeni yake ni mratibu wa kongamano Cynthia Henjewelle
 Akitaniana na wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
 Akijichagulia bidhaa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.