MWIGULU NCHEMBA AHOJIWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA

ALIYEKUWA Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Iramba magharibi (CCM),Mwigulu Nchemba amehojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Iramba,Mkoani Singida kwa muda wa zaidi ya saa mbili kwa tuhuma za kukiuka sheria ya gharama za uchaguzi na sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida,Joshua Msuya alithibitisha kuhojiwa kwa Mwigulu julai,27,mwaka huu kuanzia saa 10:30 jioni hadi saa 12:45 jioni na kwamba tukio hilo lilitokea katika zoezi linaloendelea na kura za maoni ndani ya Vyama vya Siasa.
Aidha Msuya alifafanua kuwa majukumu ya msingi ya TAKUKURU ni pamoja na kupambana na vitendo vya Rushwa kwa kuelimisha,kudhibiti,uchunguzi na Mashtaka.
“Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU anapenda kuwatahadharisha wagombea wa Udiwani na Ubunge Mkoani Singida kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye kampeni za kura za maoni”alisisitiza Msuya.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Singida tahadhari hiyo ya kutojihusisha na vitendo vya rushwa inahusisha wakati wa kipindi cha kampeni na uchaguzi mkuu wa mwezi Okt,mwaka huu kwa ajili ya kushawishi kuchaguliwa kwa nafasi wanazoomba kuteuliwa iwe niudiwani au ubunge.
Hata hivyo kiongozi huyo mkuu wa TAKUKURU aliweka bayana pia kuwa kwa wale wote watakabainika kukiuka sheria kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kutoa fedha,madawati,vifaa vya michezo au rushwa ya aiana nyingine yeyote,hawatasita kufuatiliwa kwa karibu.
Msuya hata hivyo aliweka bayana pia kwamba endapo mgombea yeyote yule atabainika kujihusisha na vitendo hivyo,hatua zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi Cap.343 R.E 2002 na sheria ya gharama za uchaguzi pia namba 6/2010.
Katika hatua nyingine Msuya alikanusha taarifa zilizoenea mjini Singida kwamba mmoja wa wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM aliikimbia gari yake baada ya kunusurika kukamatwa na TAKUKURU kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
“Lakini kwa kuwa kuna maneno maneno ya uvumi yameanza kutokea inawezekana mtuhumiwa alikuwa akifanya jambo kwani taarifa zilizopo ni kwamba mgombea huyo amekuwa akitumia muda wa usiku kuvunja sheria za uchaguzi,hivyo tunaomba ushirikiano kwa wananchi watakapobaini ukiukwaji huo wa sheria za uchaguzi”alisisitiza Msuya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.