Nipitisheni nilirejeshe Jimbo la Kawe- Pijei



Mwandishi Wetu

MTIA nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kawe, Jumaa Mhina 'Pijei', amewaomba wananchi wa Kawe kumpa kura ili aweze kulirejesha jimbo mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika kampeni zake za mwishoni jimboni humo, Pijei, alisema mbali ya kujitokeza makada 21 kulitaka jimbo hilo, wananchi ndiyo wenye uwezo wa kuamua nani wa kumpa nafasi hiyo.

"Wanachama sehemu zote tulizopita watakuwa tayari wamemwona anayefaa kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Kawe, nami naamini nafasi hiyo ninaiweza kwani vijana, akina mama na hata akina baba wanajua kazi zangu za maendeleo nilizozifanya jimboni kwetu," alisema.

Pijei katika kata zaidi ya tano za jimbo hilo, amekuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na jinsi alivyokuwa akijinadi katika mikutano ya kampeni ya kura za maoni.

Jimbo la Kawe limekuwa likishikiliwa na upinzani tangu mwaka 2010, likiwa chini ya Halima Mdee,hivyo CCM wamejipanga kuhakikisha wanalirejesha mikononi mwao, lakini kama likimpitisha mtu sahihi anayependwa na wengi.

Baadhi ya waliojitokeza ni Mtiti Butiku, Yusuph Nassoro, John Mayanja, Dickson Muze, Dk. Wilson Babyebonela, Kippi Warioba, Colman Masawe, Elias Nawera, Abdallah Majura na Jerry Muro.

ciao

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.