Rais Kikwete akabidhiwa Joho na Cheti cha Shahada ya Doctor of Laws

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akimkabidhi Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rais joho na cheti iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maprofesa waandamizi wa chuo hicho.Tayari Rais Kikwete alishatunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika Octoba mwaka 2011.
Profesa Agnes Mwakaje wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimvika kofia ya kitaaluma Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rasmi Rais Joho na cheti cha shahada ya heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akisoma maelezo mafupi baada yeye na jopo la maprofesa waandamizi wa chuo hicho kumkabidho Joho la taaluma na cheti cha Shahada ya heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) ya chu kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandakla pamoja na maprofesa waandamizi wa chuo hicho muda mfupi baada hafla fupi ya kumkabidhi Rais Joho na Cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) ikliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA