SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI

Nikukaribishe msomaji katika ukurasa wetu huu ambao tumekuwa tukijuzana mambo mengi ya msingi katika ustawi wa afya zetu.
Wiki iliyopita tuliangalia tatizo la wanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Tuliangalia sababu na dalili za tatizo hilo la mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa tukashauriana mambo ya msingi ya kuzingatia ili kuondokana na tatizo hilo.
Leo ningependa tuangalie suala la mwanamke kukosa hedhi.
Inafahamika kwamba mwanamke au msichana yeyote aliyepevuka kikamilifu, hupata siku zake za kutokwa na damu isiyoganda katika njia ya uzazi mara moja kwa mwezi. Dalili hiyo inaashiria ukomavu katika viungo vya uzazi.
Hata hivyo, kuna wakati mwanamke au msichana anapatwa na tatizo la kutokuona siku zake, hii ni dalili ya kuwepo kwa tatizo katika mfumo wake wa uzazi.
Ifahamike kwamba kukosa siku kwa mwanamke kumegawanyika katika makundi mawili.
Kundi la kwanza ni wale wanaokosa siku zao kwa kawaida bila ugonjwa na kundi la pili ni wale wanaokosa siku zao kwa sababu ya ugonjwa.
Leo nitazieleza sababu ambazo si za ugonjwa zinazoweza kumfanya mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila siku, yaani vyakula anavyokula (life style).Ulevi: Wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo kwenye hatari ya kukumbwa na tatizo hili. Lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na 49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya unywaji wa pombe kila siku
Sigara: Tatizo moja kubwa ambalo huwakumba wanawake wanaovuta sigara ni kukosa hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri wa miili yao kufanya hivyo.
Unene: Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito. Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa.
Kitaalam hali hiyo inatokana na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene au walio na uzito uliopitiliza) na homoni za kujamiiana yaani sex homones.
Kutokula nyama: Wengine ni wanawake ambao wanafanya mazoezi mazito mara kwa mara na wenye umri kati ya miaka 39 na 49 au wasiokula nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian) nao  wamo katika hatari ya kukosa kuona siku zao za hedhi.
Wengi wa wanawake wanaopatwa na tatizo hili hukumbwa pia na tatizo la kuchelewa kuacha kupata hedhi kama inavyotakiwa wakiwa katika umri unaotakiwa na hali hiyo huwahatarisha kwani wanaweza kukumbwa na hatari ya kupata saratani ya matiti.
Menopause kama tulivyoeleza hapo juu, ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiiana, hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya kujamiiana kwa mwanamke. Hali hiyo husababisha nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala, matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.
USHAURI Mwanamke yeyote ambaye ataona dalili au kutopata hedhi yake muda muafaka ni vyema akaenda kumuona daktari au akatutembelea Sigwa Herbal Clinic kwa uchunguzi na matibabu ya uhakika. Tunapatikana Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Arusha, Mwanza, Kigoma, Mbeya, ili afanyiwe uchunguzi na kama ataonekana ana tatizo la kiafya litapatiwa ufumbuzi. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA