SHIRIKA LA GLOBAL PEACE FOUNDATION (GPF) LAANDAA KONGAMANO KUBWA LA VIJANA LA KUJADILI AMANI, KUFANYIKA ZANZIBAR KUANZIA JULAI 12, 2015


  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano kubwa la vijana  litakalofanyika Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mzima kuanzia Julai 12 mwaka huu. Kongamano hilo litahudhuriwa na marais wastafu na viongozi maarufu. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi na Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa
 Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi  (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga na  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
 Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga  akizungumza katika mkutano huo.
 Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa akizungumza kuhusu kongamano hilo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha amani iliyopo ili nchi yetu isije ikakumbwa na machafuko kama nchi za jirani.

Akizungumza leo jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation na Mshauri wa Amani Afrika , Arnold Kashembe alisema Shirika hilo limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC).

"Shirika la GPF limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambao utafanyika Zanzibar kuanzia Julai 21- 24," alisema Kashembe.

Kashembe alisema mkutano huo wa kipekee utawakutanisha maraisi wastaafu nane akiwemo Keneth Kaunda na Amani Karume, viongozi wa dini, wafanyabiashara na viongozi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi jirani.

Aidha Global Peace Leadership Conference (GPLC) 2015 itatoa mafunzo na nyenzo ili kuhimiza ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujaribu kupunguza tofauti na matatizo yanayowakumba.

Mada nyingine ni kuwapongeza vijana 400 kutoka Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki kuongeza nguvu katika mbinu za ujasiriamali na kuwa mfano wa wanafunzi wa wengine huko watokapo.

Kujenga mikakati imara ya kudumisha ukaribu na kusaidiana mbinu za kupambana na umaskini, tatizo la ajira, HIV, Malaria na kuwezesha na kuzindua misheni Maendeleo ya Afrika kama lengo kuu na kiini cha mabadiliko kupitia Amani, Uongozi bora, na Uimara wa maendeleo kiuchumi.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.