SUKY CLASSIC BOUTIQUE YAINGIA MKATABA NA MEDO KUSAIDIA UTOAJI WA ELIMU MKOANI MOROGORO


 Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo Mkoa wa Morogoro, James Mbaligwe.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Suky Classic Boutique, Kiki Mussa.
  Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo Mkoa wa Morogoro, James Mbaligwe, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkataba huo walioingia na Suky Classic Boutique wa kusaidia elimu nchini
  Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo Mkoa wa Morogoro, James Mbaligwe na  Mkurugenzi Msaidizi wa Suky Classic Boutique, Kiki Mussa wakipeana mkono huku wakifurahi baada ya kuzungumza na wanahabari kuhusu jambo hilo la kusaidia changamoto za elimu kwa watoto wa kike.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (Medo), imepata udhamini wa asiliamia tano kutoka duka la nguo za kisasa la Suky Classic la Kinondoni Manyanya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa duka hilo Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Msaidizi wa  duka hilo, Kiki Juma alisema waliguswa na mradi huo wenye lengo la kusaidia mahitaji ya watoto hao ili wapate elimu.

"Tunapenda kuwasapoti watoto hawa waliochini ya mradi 
unaoendeshwa na Medo kwa kuwasaidia mahitaji muhimu kama peni. daftari, sare za shule na mahitaji mengine" alisema Juma.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro, James Mbuligwe alisema msaada huo umetolewa wakati muafaka ukizingatia ni msimu wa kufungua shule ambapo watoto hao waliochini ya mradi wanamahitaji mengi.

"Kwasasa taasisi yetu imezindua kampeni maalumu ya 'Nisaidie 500 Yatosha kunipa elimu ambapo balozi wa mradi huo ni Msanii Wastara Sajuki" alisema Mbuligwe.

Alisema wasanii na watu maarufu mbalimbali wameguswa kusaidia mradi huo ambapo Linah Sanga amejitolea kuandaa chakula cha hisani baada ya mfungo wa ramadhani kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia watoto walio ndani na nje ya mradi kujengewa kituo cha elimu mkoani Morogoro.

Alisema msanii Kajala Masanja, Mshereheshaji Pilipili na mshindi wa Big Brother Afrika kwa umoja wao wamejitolea kusaidia watoto hao kwa kuchangisha fedha kupitia mitandao yao ya kijamii kwa ajili ya kusaidia mradi huo.

Mbuligwe alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania popote walipo kuusaidia mradi huo ili uweze kuwafikia watoto wengi zaidi kote nchini.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI