TIGO YAMPONGEZA MSANII DIAMOND PLATNUMZ KWA KUSHINDA TUZO YA KIMATAIFA


indexKampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo Tanzania imesema itaendelea kusaidia maendeleo ya sanaa na utamaduni kwa kukuza vipaji vya wazawa nchini.
Tuna ari juu ya muziki na tunaamini kwamba kukuza wasanii wetu ni sehemu muhimu ya ukuaji wa sekta ya muziki nchini Tanzania,” alisema Meneja wa huduma ya Tigo music, Balla Shareeph.
Shareeph amefafanua hili leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na msanii mahiri wa Tanzania Nasibu Abdul Alias ‘Diamond Platnumz’ kuwashukuru mashabiki wake kwa msaada wao katika tuzo za msanii bora wa Afrika za MTV 2015 zilizofanyika mjini Durban, Afrika Kusini, ambapo yeye alishinda tuzo ya mtumbuizaji bora wa Afrika. Tukio hilo lilidhaminiwa na Tigo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa muziki nchini pamoja na vyombo vya habari.
Kama kampuni, tuna dhamira ya kukuza na kutangaza muziki wetu wa ndani. Tayari tumeanzisha huduma ya muziki kupitia simu za mkononi ambayo inatoa radha tofauti ya muziki usiokuwa na kikomo nchini Tanzania “alisema Shareeph
Meneja wa huduma ya Tigo music alisema: “” Kupitia huduma ya Tigo Music, wateja wetu sasa wanaweza kupata jukwaa la muziki wa kimataifa la Deezer na kufurahia nyimbo zaidi ya milioni 38 ikiwa ni pamoja na wasanii wa Afrika na Tanzania kwenye simu zao, na kompyuta.
Akizungumza na vyombo vya habari msanii Diamond Platnumz Alisema kuwa anayofuraha kwamba Watanzania maelfu kwa maelfu walipiga kura ili kuhakikisha tuzo inakuja nyumbani Tanzania.
Ninashukuru sana kwa mashabiki wangu na wote waliokuwa wakiniunga mkono kwa safari yangu mpaka kushinda tuzo ya mtumbuizaji bora katika tuzo za muziki za Afrika zijulikanazo kama MTV 2015, Platnumz alisema, akiongeza kuwa ,tuzo hii ni ya kihistoria kwa sababu ni mara ya kwanza kwa msanii wa kitanzania kushinda tuzo ya MTV.
Nashukuru kwa ushirikiano wa Tigo kwa kutangaza muziki wa kimataifa, Deezer ambao walitoa jukwaa la muziki wangu kwa ajili ya mashabiki kusikiliza na kupakua. Huduma ya Tigomusic imetoa mchango mkubwa kutanga kazi yangu kimataifa.
Alitoa wito kwa wanamuziki wa ndani kujiunga na jukwaa la Tigomusic ili kufurahia mapato zaidi na pia kuhakikisha kazi zao zinapatikana kwa mashabiki wao zaidi na kupata kutambuliwa zaidi kimataifa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA