VITUKO VYATAWALA MCHAKATO WA KUWANIA UBUNGE NDANI YA CHAMA JIMBO LA MBEYA MJINI.


 SEHEMU ya wana-CCM wa kata ya Nsalaga 
 MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, naye akipiga magoti kuomba kura 
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga  akiomba kura kwa mtindo wa kujigalagaza ardhini

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya Watia nia ya Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM wamelazimika kuomba kura kwa aina tofauti kwa wanachama wao.
Makada hao walilazimika kupiga magoti, kugalagala ardhini, kulazimisha kuulizwa maswali, ili mradi wapiga kura wawaonee huruma na kuwachagua.
Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini,walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.
Vituko hivyo vilileta bashasha na burudani ndani ya kata hiyo, na kuwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu kulazimika kusimama ili kwenda kumuinua Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa, Fatuma Kasenga, aliyekuwa anagalagala ardhini kuomba kura
Fatuma ambaye hii ni mara yake ya pili kujitokeza kuwania ateuliwe na CCM kuwania ubunge jimbo la Mbeya mjini, alisema mwaka 2010 kura zake hazikuweza kutosha hivyo kuwaomba wana-CCM wasimuangushe mwaka huu.
Aliongeza lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni kutaka kurudisha heshima ya jimbo la Mbeya, ambayo hivi sasa imepotea baada ya jimbo hilo kuwa chini ya mbunge wa kutoka chama cha upinzani kwa miaka mitano sasa.
Fatuma ambaye alikuwa akijinadi huku akiwa amepiga magoti, ambapo mara baada ya kumaliza dakika zake tatu alizokuwa amepewa pamoja na kujibu maswali aliyoulizwa, ndipo alipoanza kugalagala huku akiomba kura kwa wana-CCM.
Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu, kulazimika kusimama na kwendakumsaidia kumuinua kasha kumsindikiza walipokuwa wamepangiwa kukaa wagombea wenzake.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema wakati anachaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2012, alikuta asilimia kubwa ya vijana ndani ya jiji la Mbeya wakiwa wamekata tamaa na kuhamia upinzani.
Kajuna alisema kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwafikia vijana hao akianzia na wale wa CCM, kukaa nao na kuwauliza sababu iliyopelekea wakate tamaa na Chama, ambapo aliwaomba warudi kukitumikia na kukitetea Chama.
Mara baada ya kumaliza kujinadi kwa wana-CCM hao, Kajuna aliamua kupiga magoti na kuomba kura akiwaahidi wanachama hao kuwa anao uhakika wa asilimia nyingi kuwa anao uwezo wa kulikomboa jimbo hili, kwani ametoa misaada mingi kwa vijana, wanawake na wazee.
Kwa pande wake Mkurugenzi wa kituo cha radio Generation Fm, kilichopo jijini Mbeya, Shadrack Makombe, alisema yeye ni kijana wa viwango, hivyo kuwaomba wana-CCM wamchague ilikuipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Makombe alisema akipewa ridhaa hiyo anao uhakika wa kulikomboa jimbo la Mbeya mjini, na baada ya kutekeleza hilo atahakikisha anatafuta wafadhiri watakaojenga viwanda ili viweze kutoa ajira kwa vijana mjini Mbeya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI