Zantel yatoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania

 DSC_0032
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete akizungumza na waandishi wa habari Julai 19, 2015 wakati wa kukabidhiwa kisima kwa ajili ya kituo chake kilichopo Kimara Jijini Dar es Salaam kutoka kwa kampuni ya Zantel. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose
2
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda akizungumza wakati wa kukabidhi kisima kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Zantel, Pratap Ghose.
DSC_0038
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akisisitiza jambo wakati wa kukabidhi kisima kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
DSC_0070
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizindua kisima cha maji kilichojengwa na kampuni ya simu ya Zantel kwa ajili ya kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
DSC_0076
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifungua bomba la maji mara baada ya kuzindua kisima cha maji kilichojengwa na kampuni ya simu ya Zantel kwa ajili ya kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
DSC_0004
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose wakati wa kukabidhi kisima kilichojengwa na kampuni ya simu ya Zantel kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa leo kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makadhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka
‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshilmiwa Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.
‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.
Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.
Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.
‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*