Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya
wazee Zanzibar (JUWAZA), Mwadini Kutenga akiwakaribisha wageni wakati wa
shughuli ya makabidhino ya msaada wa chakula kutoka kwa Zantel kwenda
kwa jumuiya ya wazee Zanzibar. Kulia kwake ni NAIBU Katibu Mkuu, Wizara
ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham
Juma Khamis akifuatiwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed
Mussa.
Mkurugenzi
wa Biashara wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati wa makabidhiano
ya msaada wa chakula kutoka Zantel kwa Jumuiya ya Wazee Zanzibar.
Anayemfuatia ni NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii
,Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis na mwisho ni Naibu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazee Zanzibar (JUWAZA), Mwadini Kutenga.
NAIBU
Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake
na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis akimkabidhi msaada , Pili Ahmada wakati
wa makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Kampuni ya simu ya
Zantel kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar, kulia Mkurugenzi wa Biashara
wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti.
NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya
Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham
Juma Khamis akizungumza na wazee wakati wa kupokea msaada wa vyakula
kutoka Zantel, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed
Mussa na kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazee Zanzibar
(JUWAZA), Mwadini Kutenga.
Sehemu ya wazee waliokabidhiwa msaada wa vyakula na Zantel.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu-Zanzibar
Kampuni ya simu za mikononi ya
Zantel leo imetoa msaada wa vyakula kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani kwa
makundi maalumu ya wazee hapa visiwani Zanzibar.
Msaada huo unajumuisha sukari, unga wa ngano pamoja na mchele umetolewa katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo.
Kampuni ya Zantel upande wa
Zanzibar imeainisha wazee zaidi ya 120 wenye uhitaji wa vyakula kwenye
mwezi huu wa Ramadhani walio chini ya jumuiya ya wazee hapa Zanzibar.
Akizungumza wakati wa makabidhiano
hayo kwa wazee, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel-Zanzibar, bwana
Mohammed Mussa, amesema ni kawaida kwa kampuni ya Zantel kusaidia
makundi mbalimbali ya kijamii katika kipindi hiki cha Ramadhani.
‘Tuna furaha sana leo kuweza
kusaidia jamii hii ya wazee ambao mara nyingi wamekuwa wanasahaulika,
kwani tunaamini wazee ni sehemu muhimu sana ya jamii ndio maana Zantel
leo tumeamua kutoa msaada huu ambao unatutofautisha sana na makampuni
mengine katika vipaumbele vyetu’ alisema Mussa.
Mussa aliongeza kuwa kama kampuni
ya simu inayoongoza Zanzibar, Zantel mara zote imekuwa mfano katika
shughuli zake za kijamii na vipaumbele vyake kiujumla.
Akizungumza wakati wa shughuli
hiyo, mgeni rasmi ndugu Msham Abdallah, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar, alisema anaipongeza Zantel kwa
kushirikiana na serikali kuyasaidia makundi ya wazee.
‘Serikali imekuwa ikifanya juhudi
mbalimbali katika kulisaidia kundi hili la wazee, kwahiyo ni furaha
kwetu leo kuona Zantel imekuwa ya kwanza kusaidia kundi hili leo’
alisema bwana Abdallah.
Akitoa neno la shukrani kwa
kampuni ya Zantel, naibu mwenyekiti wa jumuiya ya wazee Zanzibar, Bwana
Mwadini Kutenga, alisema anawashukuru Zantel kwa msaada huo, akisema
umekuja kwa wakati mufaka hasa ukizingatia kuwa wanakaribia kuadhimisha
sikukuu ya Idi.
‘Kwa misaada hii, Zantel
inawafanya wazee nao wajiskie sehemu ya jamii, kwani mara nyingi
wamekuwa wakisahaulika sana na kwa hakika hatutawasau kwa ukarimu wao
huu’ alisema bwana Kutenga.
Kampuni ya Zantel imekuwa msitari
wa mbele katika kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii kipindi hiki cha
mwezi wa Ramadhani, na msaada huu ni maalumu kwa kundi la wazee ambalo
mara nyingi linasahaulika katika jamii.
Jumuiya ya Wazee Zanzibar (JUWAZA)
ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa na lengo la kuwaunganisha na kuwasaidia
wazee Zanzibar na sasa ina wanachama zaidi ya 1000.
Comments