AJALI NA VIFO VITOKANAVYO NA AJALI MKOA WA DAR ES SALAAM VYAPUNGUA


 Mkuu wa usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam, Peter Sima  katikati akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Maonesho ya usalama barabarani ya yatakayofanyika tarehe Agosti 24 na 25 mwaka huu katika viwanja vya mashujaa Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam, kulia ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi na  Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Awadhi Haji na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani, Elifadhili Mgonja.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani, Elifadhili Mgonja.
  Picha na Emmanue Massaka.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
AJALI za barabarani jijini la Dar es Salaam zimepungua katika kipindi cha nusu ya kwanza ya 2015 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa 2014.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es Salaam, Elifadhili Mgonja amesema kuwa takwimu zinaonyesha kupungua kwa ajali za barabarani 2,731 katika kipindi cha Januari -Juni 2015 zilitokea ajali za vifo 1,731 ikilinganishwa na ajali 4,462 zilizotokea kipindi cha Januari-Juni ,2014 ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 61.

Amesema kuwa ajali za vifo 87 katika kipindi cha Januari hadi juni mwaka 2015 zimeripotiwa  kwa ajali za vifo 165 ikilinganishwa na ajali za vifo 252 zilizotokea katika mwaka uliopita  ambayo sawa na asilimia 34.5.
Mgonja amesema idadi ya watu waliokufa 93 kwa 2015  katika na idadi ya ajali zilizokuwa 187 kwa ikilinganishwa  na watu waliofariki 280 katika mwaka uliopita  sawa na asilimia 33.2.

Amesema upungufu  waliojeruhiwa  1, 801 kwani mwaka huu ,waliojeruhiwa walikuwa 1,650 ukilinganishwa na mwaka uliopita wa mwaka 2014 uliokuwa na majeruhi 3,451  sawa na asilimia 52.18.
Aidha amesema kuwa wataandhimisha wiki ya usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Agasti 24 hadi 28  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU