BANK OF AFRIKA TANZANIA YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 210 KUSAIDIA MATIBABU YA WOTOTO WANAOZALIWA NA MIGUU ILIYOPINDA


  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
 Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
 Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na  Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani
kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya
CCBRT
…………………………………………..
NA  FRANCIS DANDE
 
RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana
aliongoza  matembezi ya hisani ya
kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani
kwa ajili ya kuchangia  matibabu ya
watoto waliopinda miguu.
Matembezi hayo yaliyodhaminiawa  na Benki ya Afrika – Tanzania, lengo kuu
lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia
watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni
ya  ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja
iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka  huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha  CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa
watoto  400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu
nchini kote,ilikuyabadili  maisha  yao na kuwa
ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya  Benki ya Afrika –
Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria
kurejesha kwa jamii kile  inachopata  kwa kuwa inaendesha  shughuli
zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu
wa kuhimiza  usaidizi katika suala hili
jema, kwa kuwa  CCBRT inatoahuduma kawa
jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze  kupata
matibabu,” alisema Mwanaidi .
Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza:
“ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa
Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi
chote  cha kampeni hii. Maisha ya  a mamia ya
watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na
matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha  ya watoto hao bila  kupata msaada kutoka kwa washirika wetu
wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU