CCM KUZINDUA ILANI YAKE YA UCHAGUZI AGOSTI 23 WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI


1
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari, huku akiwa ameshikilia kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Ilani hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 23 Agosti, mwaka huu, ndiyo itakayotumika kwa kipindi cha miaka 5 ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi kupitia mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote nchini Tanzania.
Nape Nnauye amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dr. John Pombe Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na kila kijiji shilingi milioni 50 "Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ".
Amefafanua na kuongeza kuwa "Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza kampeni mapema wakati hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na taratibu za uchaguzi". Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya CCM Ofisi ndogo Lumumba leo.
2
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akitolea ufafanuzi mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari wakati akizungumza nao kwenye mkutano uliofanyika CCM Lumumba jijini Dar es salaam.
3
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiionyesha ilani ya uchaguzi iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
5
Hii ndiyo Ilani yenyewe.
6
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
7
Baadhi ya wapiga picha vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio katika mkutano huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA