FILIKUNJOMBE APITA BILA KUPINGWA WAPINZANI WAKE WAINGIA MITINI NA FOMU ,MGOMBEA WA CHADEMA ASHINDWA KUJAZA TAREHE NA KUTORUDISHA FOMU MMOJA‏

fomu  ya  mgombea  wa  Chadema ubunge  Ludewa zikiwa  hazijatimia baada ya tomu ya  tamko kukosekana
Fomu ya  mgombea  wa Chadema  ikiwa haijazwa senemu ya  tarehe ,mwezi na mwaka
Mzee  Kada  wa Chadema  akimpongeza  mbunge wa  Ludewa  Deo Filikunjombe  baada ya  kupewa  barua ya kupita  bila  kupingwa
Mbunge  wa  Ludewa  Deo  Filikunjombe  akizungumza na  wanachama  wa CCM na  wananchi wa Ludewa baada ya  kupita  bila  kupingwa
Filikunjombe  akionyesha  barua ya  kupita  bila  kupingwa
Msimamizi  wa uchaguzi jimbo la  Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza  mbunge  Filikunjombe  baada ya  kumkabidhi barua ya  kupita  bila  kuingwa  ubunge jana 
Na Matukiodaima Blog
ALIYEKUWA  mbunge   wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe (CCM)  amepita  bila  kupingwa  baada ya  mgombea  wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Barthomew Mkinga  kushindwa  kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw  Wiliam Waziri alisema  jana   kuwa Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo  kumkabidhi  barua  rasmi Filikunjombe   ya kupita  bila  kupingwa
Waziri alisema   kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;
Kuwa Wagombea wa DP na TLP walishindwa  kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea   huyo  wa Chadema  aliyereja  fomu  ya  wadhamini  bila  kujaza tarehe  ,mwezi  wala mwaka ambao uchaguzi  mkuu utafanyika .
Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa TLP Bw  Blanka  Haule  alisema  kuwa alishindwa  kurejesha  fomu hizo  kwa wakati kutokana kukosa picha za  kubandika katika  fomu hiyo  kutokana na  hali ya mazingira ya  Ludewa  kukowa  eneo la  kupiga  picha hizo.
Kwani  alisema picha  ambazo alipiga  Njombe  alizisahau  alikoziweka   hivyo  kulazimika  kwenda  kupiga  pich nyingine  za  haraka kwa  muda  wa dakika tatu  ila  cha  kushangaza dakika  tatu  za kutoka  picha  hizo  zilionekana  kushindwa  kutoka kwa  wakati na kutoka  saa 11  jioni .
“Nilijipanga  kugombea  ubunge  ili  kumpokea  ubunge  Deo Filikunjombe na  kuendeleza  yale  yote  aliyoyafanya  jimboni  ila watu  wa  picha  walinikwamisha na  kushindwa kupata  picha kwa  wakati hivyo kwa  sasa  ndio  basi  tena japo ilikuwa ni  Demokrasia lakini kapita  bila  kupingwa  ndio mbunge  wetu:”
Akizungumzia  hatua ya  mgombea  wao wa Chadema  kushindwa  kukamilisha  taratibu  za  ujazaji wa  fomu  hizo Bw Daniel Songo alisema kuwa mgombea  wao hakuwa makini hata  kidogo kwani alikuwa ni mtu ambae hakutulia na muda  mwingi alikuwa akifikiria  juu ya  wanachama  wanaohama  chama na kuacha kutulia katika kujaza  fomu  hizo .
Japo  alisema chama hicho  kimepoteza  umaarufu  kutokana na  mwenendo wa  viongozi wa juu wa chama  hicho  kuendekeza  siasa za ukanda zaidi  na kuacha  kutazama uhai wa  chama   hicho.
Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Ludewa Stanle Kolimba  alisema  kuwa amepokea kwa  furaha kubwa hatua ya  mgombea  wake wa nafasi ya  ubunge  kupita  bila  kupingwa na kuwa kazi kubwa kwa  sasa  kuhakikisha mgombea  urais wa CCM Dr John Magufuli anapata  kura  za  kimbunga  pamoja na  kupigania  kata  zote kuona CCM .
Kwa upande  wake  Bw  Filikunjombe  akizungumzia hatua hiyo ya  kupita  bila  kupingwa alisema ameipokea  kwa vizuri sana kwa  alitegemea wapinzani  hao  wajitokeze  ili aweze  kuwaonyesha kazi  kwa  kuhakikisha  wanaangukia  pua katika uchaguzi huo .
Alisema kazi  kubwa ya  maendeleo ambayo ameifanya katika  jimbo  hilo kwa miaka  mitano na imani kubwa ambayo wananchi wa Ludewa wanayo dhidi yake ilikuwa ni  vigumu kwa  wapinzania hao  kupata  kura Ludewa.
Bw  Filikunjombe  aliwaomba  wananchi wa Ludewa kura  zote  ambazo  walipanga  kumpigia  yeye  kuzielekeza  kwa mgombea  Urais Dr Magufuli na kwa madiwani wa CCM na  furaha  yake  kuona wapinzani  wanaambulia  patupu katika  wilaya ya  Ludewa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI