HATIMA YA BEKI MTOGO YANGA SC NI LEO, ANAJARIBIWA DHIDI YA MBEYA CITY SOKOINE

BEKI wa kati wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou leo anatarajiwa kufanyiwa majaribio ya mwisho- wakati Yanga SC itakapocheza na Mbeya City katika mchezo wa kirafiki mjini hapa.
Baada ya kuwa mazoezini kwa wiki nzima na kumridhisha kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm- Bossou leo atachezeshwa katika mchezo dhidi ya Mbeya City.
Iwapo beki huyo ataonyesha kiwango zuri leo dhidi ya Mbeya City inayoongozwa na mshambuliaji mkongwe, Themi Felix Buhaja anaweza kupewa Mkataba. 
Vincent Bossou aliyezaliwa Februari 7, mwaka 1986 mjini Kara, Togo, aliibukia klabu ya Maranatha FC ya kwao, kabla ya kusaini Etoile du Sahel ya Tunisia Januari 15, mwaka 2010 Mkataba wa miaka miwili.
Vincent Bossou ataichezea Yanga SC dhidi ya Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Hata hivyo, Mkataba wa 'sentahafu' huyo Etoile Sportive du Sahel ulivunjwa baada ya miezi mitatu tu naye akarejea Maranatha FC Machi 18, mwaka 2010.
Mei mwaka 2011 akaenda kusaini klabu ya Navibank Saigon FC ya Vietnam, kabla ya kuhamia Becamex Binh Duong, baadaye TDC Binh Duongzote mwaka 2013, An Giang mwaka 2014 na Goyang Hi FC mwaka jana.
Alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo kilichojitoa AFCON ya mwaka 2010 Angola baada ya basi la wachezaji kushambuliwa na majeshi ya waasi ikiwa njiani kuelekea kwenye fainali hizo.
Bossou, ambaye ameendelea kuwa mchezaji wa Togo hadi mwaka huu, aliwahi ‘kumvimbia’ Nahodha wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba wakati wa mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika baina ya Ivory Coast na Togo Uwanja wa Royal Bafokeng Januari 22, 2012 mjini Rustenburg, Afrika Kusini.
Yanga SC inasaka beki wa kiwango cha juu ili kuimarisha ukuta wake katika vita za ubingwa wa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa sasa, Yanga SC ina mabeki wanne wa kati wote wazawa, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati pia kiungo Mbuyu Twite raia wa DRC anaweza kucheza nafasi hizo.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*