MSAMA PROMOTIONS KUANDAA TAMASHA LA KUIOMBEA TANZANIA INAYOELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUU

Mkurugenzi wa Msama Promotions akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo,jijini Dar kuhusiana na kuandaa tamasha la kuiombea Tanzania inayoelekea kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika,Oktoba 25 mwaka huu,Tamasha hilo linatarajia kufanyika Oktoba 4.

KAMPUNI ya Msama Promotions imeandaa Tamasha kubwa la kihistoria ambalo halijawahi kufanyika nchini la kuiombea Tanzania inayoelekea katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama Tamasha hilo litafanyika Oktoba 4, jijini Dar es Salaam.

Msama alisema kutokana na uzito na heshima ya tamasha hilo, linatarajia kushirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wa ndani na nje ya nchi ambao wanaotamba katika tasnia ya muziki huo.

Alisema japo ni mara ya kwanza kwa kampuni yake kuandaa tamasha kama hilo katika historia ya uchaguzi nchini, anaamini kwa vile amani ni kitu muhimu katika uchaguzi, wengi watamuunga mkono.
Msama alisema anaamini wengi watajitokeza kuungana pamoja na viongozi wa kitaifa na kada mbalimbali kuuombea uchaguzi huo ambao ni njia ya kidemokrasia ya kupata viongozi kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani.

“Watanzania wajiandae kuiombea amani Tanzania kupitia muziki wa Injili hasa waimbaji mbalimbali wa kutoka nje ya Tanzania watashiriki katika tukio hilo ambalo bado tuko katika mchakato wa mahali tutakapofanyia,” alisema Msama na kuongeza:

“Tamasha hilo kubwa kimaudhui linakaribia Tamasha kubwa la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu mwaka 2000,” alisema Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili.

Aidha Msama alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, watahamishia maombi hayo katika majiji mengine manne kwa lengo hilo la kuombea amani na utulivu uchaguzi Mkuu.   

Alitaja nchi watakazotoka waimbaji watakaosindikiza maombi hayo niAfrika Kusini, Rwanda, Kenya, Uganda, Zambia, Burundi na DR Congo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*