NJEMBA WAZICHAPA KAVUKAVU STENDI


Njemba hao wakizichapa.
NJEMBA wawili ambao ilisemekana ni wapiga debe, wamejikuta wakizichapa kavukavu wakigombea mzigo wa abiria.

Wakizidi kunyukana
Tukio hilo lililojaza watu ambao walikuwa wakishangilia wakati njemba hao ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja wakizichapa, lilitokea hivi karibuni majira ya saa 6 mchana ndani ya kituo cha Mabasi cha Nyegezi, jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa hao walitofautiana baada ya abiria mmoja kushushwa na daladala ambapo walianza kugombea mzigo wake.

Wakiamuliwa
“Walikuwa wakigombea mzigo wa abiria sasa huyu mwenye T-Shirt ya njano alionekana kumzidi nguvu mwenye T-Shirt nyeusi, kuona hivyo, mwenye T-Shirt nyeusi alimtwisha mwenzake kichwa cha uso hadi kumtoa nundu,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:
“Baada ya jamaa (mwenye T-Shirt nyeusi) ku-’wini’ kihivyo, alimchukua abiria na mzigo wake wakaondoka na kumuacha mwenzake (mwenye T-Shirt ya njano) akijichua nundu yake.
“Nundu ilikua kwa kasi kiasi cha kuwafanya wapiga debe wenzake waanze kumcheka ambapo alipatwa hasira sana akaanza kumsaka mwenzake ili alipize kisasi,” alisema shuhuda.

Akiendelea kusimulia shuhuda huyo alisema baada ya kumsaka huku na kule, alibahatika kumuona katika duka moja akinywa maji, hapohapo alimvaa mpaka chini akaanza kumshushia ngumi za uso ambapo mwenzake huyo hakukubali alianza kurudisha mashambulizi ikawa bonge la timbwili.
Hata hivyo, mashuhuda wakiwemo wapiga debe wenzao, waliingilia kati kwa kumchukua mwenye T-Shirt nyeusi kumpeleka eneo jingine na kumuacha mwenye T-Shirt ya njano akimtangazia mwenzake kuwa hiyo vita haijaishia hapo, itaendelea siku nyingine!

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.