RFB YAFANIKIWA KUFANYA MABORESHA YA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI NCHINI


unnamed (100)
Meneja Mfuko wa Barabara Bw.Joseph Haule akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni alipokuwa akiwasilisha ripoti ya mafanikio ya utekelezaji wa Mfuko wa Barabara kwa  Serikali ya awamu ya nne.
unnamed101
Naibu Meneja Masuala ya Kiufundi Bw. Ronald Lwakatare kutoka Taasisi ya Mfuko wa Barabara akizungumza na waandishi  wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo
Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini(RFB) imefanikiwa kufanya maboresha ya barabara kwa kiwango cha lami katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nne wa Mhe. Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam Jana Bw.  Joseph Haule amesema kuwa matengenezo hayo yamefanikisha ujenzi wa  barabara kuu  zinazounganisha mikoa mbalimbali nchini kukamilika kwa asilimia 89 huku zile za Wilaya na Miji kwa asilimia 57.  
“ kazi kubwa ya Mfuko huu ni kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali   ikiwemo tozo za barabarani na  ushuru wa mafuta na baadaye  kuzigawa kupitia taasisi zinazohusika na ujenzi wa barabara ikiwemo TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya Waziri Mkuu “ alisema  Bw. Haule
Aidha aliongeza kuwa  Mfuko huo umefanikisha ujenzi wa daraja  la Mabatini jijini Mwanza ,daraja la Mwanhunzi  na daraja la Mbutu  linalounganisha Igunga na Shinyanga   pamoja na ununuzi wa vivuko  kikiwemo kile cha Mv Malagarasi.
Mbali na hayo Bw.Haule aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kuhakikisha barabara  zinatunzwa  kwa  kudhibiti magari ya mizigo yanayozidisha uzito unaochangia uharibifu wa barabara  kwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kamera  utakaokuwa unaratibiwa na mfuko huo.
Mfuko huo  umefanikiwa  kuanzisha ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe ambao ni wa gharama nafuu na wa kudumu kwa muda mrefu,hata hivyo miradi hiyo imeanza kutekeleza katika mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Kutokana na mtandao wa barabara  kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara imesaidia kuongeza ubora wa barabara na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani ikiwemo Zambia,Malawi,Burundi,Rwanda na Uganda.
Mbali na mafanikio hayo Mfuko huounakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa bajeti kutokana na fedha zinazopatikana kutokukidhi  mahitaji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA