SHEREHE YA WASANII KUMUAGA RAIS KIKWETE YAFANA DAR

 Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akitoa shukrani kwa niaba ya wasanii wenzie kwa Rais Jakaya Kikwete kwa mchango mkubwa alioutoa kwa wasanii nchini, wakati wa hafla ya kumuaga rais huyo, usiku wa kuamkia leo  kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick (kushoto) wakiungana na wasanii kucheza muziki wakati wa hafla hiyo.
 Mafataki yakipigwa ikiwa ni moja ya shamra shamra za hafla hiyo ya wasanii kumuaga Rais Kikwete.
 Rais Kikwete akisalimiana na Meneja wa Kimataifa wa Msanii Naseeb Abdul 'Diamond' (katikati) wakati wa hafla hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwa wamemuweka kati Mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini  kupitia CCM, Hussein Bashe walipokutana wakati wa hafla hiyo.
 Komredi Kinana akisalimiana na msanii wa filamu JB
 Rais Kikwete akiwa na Dk. Magufuli pamoja na Komredi Kinana
 Rais Jakaya Kikwete akiwa na Komredi Kinana na Nape Nnauye

Wasanii wa fani mbalimbali jana kuanzia jioni walijumuika na Rais Jakaya Kikwete katika chakula cha jioni, kwa ajili ya kuagana naye, kufuatia kukaribia kumaliza mda wake wa urais.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, pamoja na Rais Kikwete, ilihudhuriwa pia na Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza kuwa wasanii ni watu muhimu ambao kazi zao zinapaswa kulindwa ili ziwanufaishe kama ilivyo kwa wasanii wengine duniani kama walioko nchi kama za Marekani.

Rais Kikwete aliahidi kuendelea kusaidia juhudi za kuwafanya wasanii waishi maisha yaliyo bora kwa kupata kipato kinacholingana na kazi zao hata akishastaafu nafasi yake ya urais.

Ili kutekeleza azma yake hiyo, Rais Kikwete aliahidi kuwa mlezi wa wasanii ili kuwewezesha masuala yao mengi yapige hatua zaidi.

Mapema wasanii walimtawaza Rais Kikwete kuwa Shujaa wao, na kumtunuku picha maalum iliyonakshiwa karibu majina ya wasanii wote nchini, Picha hiyo alikabidhiwa na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nikki wa Pili ambaye kabla ya tukio hilo, alieleza jinsi tasnia ya sanaa, inavyochangia pato la taifa na changamoto zinazowakabili wasanii.

Katika hafla hiyo, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walichangamsha ukumbi, baada ya kupanda jukwaani na kuzicharaza ala za muziki kwa umahiri mkubwa.

Dk. Magufuli aliamsha hoihoi ukumbini kwa kuzicharaza tumba, huku Napa akicharaza gita zito la Bess, na wote kuunogesha moja ya nyimbo za zamani, wa DDC Mlimani Park  ulioimbwa na msanii, Recho.

Baadhi ya wasanii wengine waliotumbuiza ni Farid Kubanda (Fid Q), Shakila, Rud, Jose Mara.


 Wasanii wakipiga makofi Rais Kikwete alipowasili ukumbini
 Rais Kikwete akisalimiana na Hussein Jumbe mwimbaji wa Bendi ya DDC Mlimanj Park 'Sikinde'
 Rais Kikwete akizungumza na Mgombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia CCM, Davis Mosha
 JK akisalimiana na wasanii
 Mtoto ambaye alikuwa ni mmoja wa waalikwa kwenye hafla hiyo akitumia simu kupiga picha na JK
 Mmoja wa wasanii akitumia simu yake kupiga picha na Rais Kikwete
 Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Dk. John Magufuli (kushoto), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa gazeti la Jambo Leo, Benny Kisaka walipokutana kwenye hafla hiyo.
 JK akisalimiana na wasanii

 JK akisalimiana na akina dada wasanii
 JK akipiga picha na wasanii
 JK akiendelea kusalimiana na wasanii

 Mwimbaji mkongwe wa taarabu, Bi Shakila Said akitumbuiza kwa wimbo wa taarabu wakati wa hafla hiyo ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kumkaribisha Dk. John Magufuli anayegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akikabidhiwa picha maalum yenye majina ya wasanii karibu wote, kutoka kwa Msanii Nickson Simon 'Nikki  wa Pili, wakati wa hafla iliyoandaliwa na wasanii kumuaga Rais huyo anayemaliza kipindi chake cha pili,kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.. Kulia ni Farid Kubanda 'Fid Q'.

 Alikiba akitoa naye shukrani kwa Rais Kikwete kwa kuwajali wasanii nchini
 Dk. Magufuli akipiga tumba huku Nape Nnauye akipiga gita kunogeza hafla hiyo ya wasanii
 Msanii Wema Sepetu akimtunza dola Dk Magufuli
 JK akishiriki kucheza muziki
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (aliyevaa kapelo) akiwa katika hafla hiyo ya wasanii kumuaga Rais Jakaya Kikwete
 Wasanii wakiwa katika hafla hiyo
 Ni muziki kwa kwenda mbele
Akina dada wakiwa wamenogewa na muziki

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI