SUGU, NATURE, PROFESSA J KUFANYA SHOO YA KUHAMASISHA MASHABIKI KUPIGA KURA OKTOBA 25, 2015


Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule “Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.
 Baadhi ya wasanii watakaowasha moto Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Mwandishi wa habari wa Times Fm, akifanya mahojiano na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J”.
Na Mwandishi Wetu.
Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota wa Bongo Movie watafanya onyesho la bure Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Wasanii hao wataongozwa na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule “Professa J” na Kara Jeremiah.
Wengine ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa 8.00 mchana ni Msaga Sumu, Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na Auntie Ezekiel.
Akizungumza jijini jana, Professa J alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya onyesho hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi bora wan chi hii wataodumu kwa miaka mitano.
Professa alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa mashabiki wao kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao kumchagua kiongozi wanayemtaka.
“Tumejiandaa vilivyo kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha mashabiki wetu kufanya kile wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya kikatiba,” alisema Professa J.
Alisema kuwa mbali ya Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika katika mikoa mengine mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano huo, Nature aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu hiyo ambayo wasanii wameamua kuitoa.
“Hii siyo kampeni ya kisiasa, sisi ni wasanii tumeamua kujitolea kufanya kazi ambayo wasanii wengi duniani wameifanya, lazima tutumie kazi yetu kutoa elimu kwa mashabiki ili wajue wajibu wao katika mambo mbali mbali pamoja na uchaguzi mkuu,” alisema Nature.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA