TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

RPC MSANGIJESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUJIFANYA | 
WATUMISHI WA JESHI LA POLISI WILAYA YA KYELA.
TUKIO LA KWANZA.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUJIFANYA | 
WATUMISHI WA JESHI LA POLISI WILAYA YA KYELA.
KATIKA TUKIO HILO WATU WAWILI OSCAR FRIDAY [20] NA SHAURI REUBEN [26], WOTE WAKAZI WA ENEO LA MIKUMI WILAYA YA KYELA WALIKAMATWA BAADA YA KUJIFANYA NI WATUMISHI WA JESHI LA POLISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 31.07.2015 MAJIRA YA SAA 12.00HRS ENEO LA STENDI YA MABASI, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAKAMANI. AIDHA WATUHUMIWA HAO WALIKUTWA NA BARUA YENYE KICHWA CHA HABARI “ KULIPIA KWA KUPEWA NAFASI YA JESHI” BARUA HIYO YENYE MUUNDO WA KIOFISI NA ANUANI ZISIZO SAHIHI ZA JESHI LA POLISI AMBAYO WALIKUWA WANAITUMIA KUTAPELI WATU KWA KUWALAGHAI KUWA WAMETUMWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KUSAMBAZA FOMU ZA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA AMBAYO INATOLEWA KWA MALIPO YA TSHS 2,000/=.
BAADHI YA MAHITAJI YALIYOMO KATIKA BARUA HIYO NI PAMOJA NA 1. MCHANGO WA BIMA YA AFYA TSHS 20,000/= 2. MCHANGO WA KUPEWA JINA TSHS 40,000/= 3. MCHANGO WA KUTHIBITISHA JINA TSHS 15,000/= 4. MCHANGO WA KUPEWA TIKETI TSHS 20,000/= 5.MCHANGO WA PICHA PASIPOTI SIZE TSHS 15,000/= NA 6. MCHANGO WA KUINGIZIWA NYARAKA ZAKO TSHS 15,000/=.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI NA KUNDI HILO LA WATU MATAPELI WANAOJIPATIA FEDHA KWA NJIA ZA HILA KWA KUTUMIA KIVULI CHA JESHI LA POLISI KWANI HAKUNA GHARMA YOYOTE KUPATA AJIRA ZA JESHI LA POLISI, HIVYO WAJIEPUSHE NA WATU HAO WANAOPITA MITAANI NA KUWARUBUNI. AIDHA KAMANDA MSANGI AMEELEZA KUWA JESHI LA POLISI NCHINI LIMEKUWA LIKIAJIRI VIJANA WENYE SIFA MBALIMBALI KADRI YA MAHITAJI YANAVYOJITOKEZA NA KWAMBA AJIRA HIZO ZIMEKUWA ZIKITOLEWA KWA VIJANA WANAOHITIMU KIDATO CHA NNE, KIDATO CHA SITA, WENYE TAALUMA MBALIMBALI NA WALE WANAAOHITIMU MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
KAMANDA MSANGI AMESISITIZA KUWA JESHI LA POLISI HUTOA MATANGAZO KWENYE TOVUTI YA POLISI www.policeforce.go.tz,REDIO MBALIMBALI, MAGAZETI NA VITUO VYA POLISI PINDI LINAPOTAKA KUAJIRI, KWA MWAKA HUU 2015 UTARATIBU NA MCHAKATO WA AJIRA ULIANZA MWEZI MEI AMBAPO VIJANA WA JKT KAMBI ZA JKT ITENDE NA ITAKA WALISAILIWA NA TIMU YA MAAFISA KUTOKA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI DSM NA ZOEZI HILO LILIHITIMISHWA TAREHE 9-10 MWEZI JULAI KWA VIJANA WA KIDATO CHA NNE NA SITA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MBEYA NA KWAMBA ZOEZI HILO LIMEKWISHA.
HATA HIVYO KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WATU WA NAMNA HIYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA HARAKA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
Imetolewa na.
AHMED .Z. MSANGI – SACP
KAMANDA WA POLISI [M] MBEYA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU