Wananchi Wamzuia Mgombea Mwenza wa CCM Barabarani Mwanga

Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo. Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo. Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya kuendelea na safari yake.
 Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya kuingia njia panda. 
Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao.
 Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*