ARSENAL YAJIONGEZEA PUMZI ULAYA, BARCELONA ‘YAENDELEZA SIFA’, CHELSEA YAPIGA MTU 4-0 UGENINI

MATOKEO NA RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Jana Novemba 24, 2015
Bayern Munich 4-0 Olympiakos
Arsenal 3-0 Dinamo Zagreb
Barcelona 6-1 Roma
Lyon 1-2 KAA Gent
FC Porto 0-2 Dynamo Kyiv
Maccabi Tel Aviv 0-4 Chelsea
Zenit St Petersburg 2-0 Valencia CF
BATE Borisov 1-1 Bayer 04 Leverkusen
Leo Jumatano; Novemba 25, 2015
FC Astana Vs Benfica (Saa 3:45 usiku)
CSKA Moscow Vs VfL Wolfsburg (Saa 1:00 usiku)
Shakhtar Donetsk Vs Real Madrid (Saa 3:45 usiku)
Manchester United Vs PSV (Saa 3:45 usiku)
Malmo FF Vs Paris Saint-Germain (Saa 3:45 usiku)
Juventus Vs Manchester City (Saa 3:45 usiku)
Borussia Monchengladbach Vs Sevilla (Saa 3:45 usiku)
Atletico Madrid Vs Galatasaray (Saa 3:45 usiku)

Alexis Sanchez akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Arsenal jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

TIMU ya Arsenal imejiongezea uhai katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-0 usiku wa kuamkia leo dhidi ya Dinamo Zagreb Uwanja wa Emirates mjini London.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mesut Ozil dakika ya 29 na Alexis Sanchez mawili dakika ya 33 na 69.
Ushindi huo unaifanya The Gunners ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi tano, lakini inaendelea kushika nafasi ya tatu Kundi F nyuma ya Olympiakos yenye pointi tisa na Bayern Munich pointi 12.
Arsenal sasa itabidi iifunge Olympiakos katika mchezo wa mwisho ili kupata nafasi ya kutinga 16 Bora.  
Mechi nyingine ya kundi hilo usiku wa jana, Bayern Munich wameitandika Olympiakos 4-0 mabao ya Douglas Costa de Souza dakika ya nane, 
Robert Lewandowski dakika ya 16, Thomas Muller dakika ya 20 na Kingsley Coman dakika ya 70 Uwanja wa Allianz Arena.
Kiungo wa Chelsea, Oscar akiwa ameweka mpira tumboni kushangilia bao lake jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Chelsea imeweka hai matumaini ya kutinga 16 Bora baada ya ushindi mnono wa ugenini wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika mchezo wa Kundi G, mabao ya 
Gary Cahill, Willian Borges Da Silva, Oscar dos Santos Emboaba Junior na Kurt Zouma Uwanja wa 
Haifa.
Chelsea sasa inaongoza Kundi G kwa pointi zake 10, sawa na FC Porto pia – lakini bado watahitaji pointi tatu katika mchezo wa mwisho kujihakikishia kuipiku Maccabi yenye pointi nane.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Dyanmo Kyiv jana imeshinda ugenini nchini Ureno mabao 2-0 dhidi ya FC Porto, mabao ya Andriy Yarmolenko kwa penalti dakika ya 35 na Derlis Gonzalez dakika ya 64 Uwanja wa Estadio do Dragao.
Lionel Messi akimlamba chenga kipa wa Roma kuifungia bao la pili Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Mabingwa watetezi, Barcelona wameendelea kung’ara baada ya kuitandika AS Roma mabao 6-1 Uwanja wa Camp Nou na kufikisha pointi 13 Kundi E.
Luis Suarez alifunga mabao mawili jana dakika ya 15 na 44, wakati mengine yamefungwa na Lionel Messi dakika ya 18 na 59, Gerard Pique dakika ya 56 na Adriano Correia, wakati la Roma limefungwa na Edin Dzeko dakika ya 91.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, BATE Borisov imelazimishwa sare ya 1-1 na Bayer 04 Leverkusen bao lake likifungwa na Mikhail Gordeychuk dakika ya pili, kabla ya Admir Mehmedi kuwasawazishia wageni dakika ya 68 Uwanja wa Borisov Arena.
Roma na Bayer Leverkusen sasa zitaingia kwenye mechi za mwisho kuwania kuungana na Barca kwenda 16 Bora, sasa zote kila moja ikiwa na pointi tano.

Douglas Costa akiifungia Bayern Munich bao la kwanza jana dakika ya nane tu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Zenit St Petersburg imeshinda 2-0 dhidi ya Valencia CF katika mchezo wa Kundi H mabao ya 
Oleg Shatov na Artem Dzyuba Uwanja wa 
Petrovski na kufikisha pointi 15, ikifuatiwa KAA Gent pointi saba na Valencia pointi sita, wakati Lyon ina pointi moja.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, KAA Gent imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Lyon, mabao yake yakifungwa na Danijel Milicevic dakika ya 32 na Kalifa Coulibaly dakika ya 95 Uwanja wa Stade de Gerland, baada ya wenyeji kutangulia kwa bao la Jordan Ferri dakika ya saba.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.