Baada ya Azam FC kumkaribisha Ivo Mapunda kufanya mazoezi na timu yao, kocha wa Azam FC kaamua haya (+Audio)

Mwezi August mwaka 2015 siku chache kabla ya dirisha la usajili la Ligi Kuu sokaTanzania bara halijafungwa, golikipa wa muda mrefu katika soka aliyewahi kucheza katika vilabu kadhaa ndani na nje ya Tanzania Ivo Mapunda alikuwa hajui hatma yake ndani ya klabu yake ya Simba, licha ya kuwa walikuwa wamempa dau la awali la usajili.
Stewart
Kocha wa Azam FC Stewart Hall
Simba walimtema Ivo Mapunda siku chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, tukio ambalo lilipelekea golikipa huyo kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu na kuishia kufanya mazoezi binafsi, kabla ya kuamua kuomba uongozi wa klabu ya Azam FCwampe nafasi ya kufanya mazoezi wakati akiwa anasubiri mipango yake ya kujiunga na klabu ya AFC Leopard ya Kenya ikae sawa.
“Ni kweli Ivo alikuja Azam FC na kuomba uongozi umpe nafasi ya kufanya mazoezi wakati ambao alikuwa akisubiria mipango yake ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, lakini kilichotokea ni kuwa kocha ameonesha kuvutiwa na uwezo wake, kwa hiyo kinachoendelea sasa hivi kati ya Ivo na Azam FC ni mazungumzo ambayo yanaendelea vizuri” >>>> Jafari Iddi
Ivo-Mapunda-making-save
Ivo Mapunda akionesha uhodari wake wa kulinda goli lake
November 25 uongozi wa Azam FC kupitia kwa afisa habari wake Jafari Iddi Magangaumethibitisha kocha wao mkuu wa klabu hiyo muingereza Stewart Hall kuvutiwa na uwezo wa golikipa huyo, hivyo ameomba uongozi wa Azam FC kumsajili golikipa huyo ili waongeze nguvu kikosi chao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.