TAARIFA YA IKULU YA KUAPISHWA KWA WAZIRI MKUU MAJALIWA

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemwapisha Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sherehe za uapisho zimefanyika leo asubuhi katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai na  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman
Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mshimiwa Pandu Ameir Kificho, Mawaziri wakuu wastaafu, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wabunge.
Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameapishwa kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na jina lake kupelekwa bungeni ambako wabunge wamelithibitisha kwa asilimia 73.5.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jioni (Novemba 20, 2015) anatarajiwa kuhutubia na kulizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.

Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
 IKULU.

20 Novemba, 2015

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA