WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NCHINI KUTEMBEA WAGENI WA KIMATAIFA MAKUMBUSHO YA TAIFA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye ukumbi wa Sanaa, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Michoro ya Mapangoni kutokwa kwa Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi Agnes Gidna.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Chimbuko la mwanadamu kutokwa kwa Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Amandus Kweka. Fuvu lilipo kulia kwenye sanduku lililo nakshiwa na dhahabu ni la Zinjanthropus lililo gunduliwa zaidi ya miaka milioni 1.7 iliyo pita huko Ngorongoro Oldvuvai kwenye miaka ya 1959. 
Balozi Mulamula akiagana na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure baada ya kumaliza kuitembelea Makumbushi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akitembezwa kujionea miundombinu ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Bw Achiles Bufure.


Na Sixmund J. Begashe
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeridhishwa na huduma mbali mbali zinazo tolewa na Makumbusho ya Taifa kwa wageni mbali mbali wanao tembelea Makumbusho hizo ili kujionea na kujifunza mambo mbali mbali yanayo huyu Tanzania.

Akiwa kwenye ziara ya kimafunzo katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mukamula amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuitumia Makumbusho za Taifa ili kutoa elimu kwa wageni mbali mbali wanaotembelea Tanzania.

Ameongeza kuwa Wizara yake hupokea wageni wengi wa kimataifa wanaokuja kwa shughui za kiserikali hivyo ofisi yake itafanya utaratibu wa kuhakikisha wageni hao wanatembelea makumbusho kwa maana ndio sehemu pekee wanapo weza kuifahamu Tanzania kwa muda mfupi bila kuizunguka nchi yote.

“Nimekuja mwenye kujionea na kujifunza huduma mnazo toa hapa, ili nijiridhishe kwanza kabla ofisi yangu haijaanza kuwaleta wageni hapa, kiukweli nimeridhishwa sana na huduma yenu na licha ya kujifunza nimeona vipo vivutio vingi vinaweza kuwavutia wageni wa kiserikali na kujifunza kupitia vitu hivi, hongereni sana” Alisema Balozi Mulamula.

Akimshukuru Balozi Mulamula kwa kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure alisema kuwa amependezwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuona umuhimu wa kuitumia Makumbusho kama Mwalimu Mwelekelezi wa Mambo yanayo thaminiwa na watanzania

“Viongozi wetu wa kubwa wakienda kikazi nchi za wenzetu, wakifika huko hutembezwa Makumbusho, ili kuwafanya wasiondoke bila kuzifahamu hizo nchi kihistoria na hata kimaendeleo ya kisayansi na teknolojia, vivyo hivyo wanapokuja hapa nchini wanapaswa kutembezwa Makumbusho ili wapate sura sahihi ya nchi yetu” Aliongeza Bw Bufure.

Mkurugenzi huyo wa Makumbusho ametoa  wito kwa Wizara zote za Serikali, Taasisi za watu binafsi na Watanzania kwa ujumla wenye kutembelewa na wageni kutoka nje ya Tanzania kuwa na Utamaduni wa kuwatembeza wageni wao Makumbusho ili kujifunza mambo ya Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*