BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA AKABIDHI GARI YA HUDUMA YA DHARURA KWA WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU


1
Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakikata utepe  wakati balozi huyo alipokabidhi gari la Ambulance kwa Waziri Ummy Mwalimu  kwa ajili ya kituo hicho.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akijaribu kuwasha gari hilo la kubebea wagonjwa lililotolewa kwa kituo hicho.
3
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba kulia na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele.
4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ,  Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba pamoja na viongozi mbalimbali wa Kituo cha kuratibu matukio ya Sumu  nchini na Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa makabidhiano hayo.
……………………………………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Dae es Salaam
Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba amekabidhi Gari la huduma ya dharura (AMBULANCE) kwa Kituo cha Uratibu wa Matukio ya Sumu nchini kilichopo chini ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Balozi huyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu sambamba na kuzindua Cheti cha Ithibati cha kuitambulisha Maabara hiyo kimataifa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo Balozi Yoshiba amesema kuwa Jumuiya ya Zimamoto ya nchini Japan imetoa magari 83 kwa Tanzania ikiwemo magari 10 ya huduma ya dharura kwa nia njema na pia kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Nchi ya Japani.
Amesema Jumuiya hiyo ilianza kutoa magari hayo tangu mwaka 2006 na kuahidi kuendeleza uhusiano huo wa kirafiki wenye manufaa kati ya Tanzania na Japani.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa makabidhiano ya gari hilo yameleta hamasa kwa upande wa Wakala na Wadau wengine katika kukabiliana na matukio ya Sumu nchini.
“Ili Taasisi iweze kufanya kazi kwa ufanisi uwepo wa miundo mbinu kama vifaa ikiwemo mitambo, vitendea kazi kama vile magari na majengo bora ni suala ambalo halina budi kupewa kipaumbele”alisema Waziri Ummy.
Pia Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa majukumu yanayotekelezwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kulinda afya, mazingira  na usalama kwa watu na hivyo kuleta utengemano katika jamii.
Aidha, Waziri Ummy amezindua cheti cha Ithibati chenye namba ISO 1705:2005 kinachoitambulisha maabara ya Mkemia Mkuu kimataifa.
Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa agizo kwa Wakala wa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa kipaumbele suala la Madaya ya Kulevya kwa kuwapima watoto haswa wa shule za msingi na sekondari ili kuweza kupambana na janga hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*