MAMBO SAAAFI, SIMBA YAANGIZA NYASI BANDIA CHINA



Mambo yakikaa sawa basi baada ya miezi michache mno, Simba itakuwa na uwanja wake bomba wa mazoezi wenye kiwango kizuri kwa ajili ya kujifua na michuano mbalimbali.
Iko hivyo kwa kuwa wiki iliyopita tayari uongozi wa Simba umefanya mawasiliano na moja ya kampuni za nchini China na kuwapa oda ya kuwatengenezea nyasi bandia ‘kapeti’ kwa ajili ya uwanja wao uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar.

Tayari kila kitu kimekamilika na kampuni hiyo imewaeleza kwamba takriban baada ya wiki tatu kila kitu kitakuwa tayari na mzigo utatumwa mapema mno.

Wakati hayo yakiendelea juzi Jumamosi, Rais wa Simba, Evans Aveva na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, walikwenda kutembelea kiwanja hicho kuangalia kinachoendelea baada ya kuamuru kufanyika kwa matengenezo ya awali kwa kuuweka sawa udongo huo wa uwanjani hapo kisha mengine yafuate.

“Tumeshaagiza hizo nyasi na kila kitu kinakwenda sawa, kwa kuanzia ni kutafuta ‘pitch’ ya kuchezea kwanza kisha mengine kama uzio yatafuata. Baada ya kufika kwa nyasi, utengenezwaji na uwekwaji wa nyasi hizo huchukua kama siku sita mpaka 10.


“Kwa hiyo kwa mahesabu hayo unaweza kuona inaweza kuchukua kama mwezi na nusu hivi na tunayoyapanga yakakaa kama tunavyotaka,” alisema Hans Poppe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.