MTANZANIA AUAWA KWENYE CASSINO NAIROBI, KENYA



Kilimanjaro
Image captionMtanzania huyo alitoka mkoa wa Kilimanjaro
Raia wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada yake kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari.
Alijaribu kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema.
Ni hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa kasino mtaa wa Eastleigh.
Kamari
Image captionMwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari
Mlinzi wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga kisu na kumuua.
Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.
Polisi wamesema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kama John Barnabas mwenye umri wa miaka 28 anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Alikuwa akifanya kazi kama fundi wa viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.
Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye wanasema alikuwa ameuza pikipiki hiyo ili kupata pesa za kwenda kucheza kamar

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.