Fastjet yatoa ofa nauli za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza


Dar es Salaam, 

Shirika la ndege la bei nafuu, fastjet, limetangaza punguzo la nauli la sh. 22,000/- kwa mwezi huu wa Aprili kwenye safari zake za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza.

Kulingana na Afisa Masoko na Uhusiano wa Umma wa fastjet, Lucy Mbogoro, ofa hiyo ijulikanayo kama JET10 imeanza kuanzia mwanzo wa April na itamalizika tarehe 30 Aprili 2016.

“Ofa hii kutoka fastjet inaashiria kwa mara nyingine tena jinsi shirika letu linavyosikiliza matakwa ya wateja wake”, alisema Mbogoro.

Mbogoro alisema kwamba wateja wanaweza kilipia nauli zao kupitia mitandao ya Tigo-Pesa, Airtel Money, M-Pesa and pia kupitia NMB Mobile Cash katika tawi lolote la Benki ya NMB.

“Wateja wanashauriwa kukata tiketi mapema ili kufurahia nauli za bei nafuu zaidi na pia wanaweza kulipia kupitia m.fastjet.com or www.fastjet.com.” alishauri Mbogoro.


Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.