JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU WA MAHAKAMA YA CHINA MHE. ZHANG JIANNAN LEO JIJINI DAR ES SALAAM.


 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa ameongozana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan (kuahoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Zhang Jiannan pamoja na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwenye Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano baina ya Mahakama ya Tanzania na China. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisalimiana na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya kuwakaribisha   Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China uliolenga kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa Mahakama za Tanzania na China leo jijini Dar es salaam. 
 Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China.
   Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wale wa Mahakam Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakibadilisha uzoefu wa shughuli za kimahakama na masuala mbalimbali ya utendaji wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China jijini Dar es salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akimweleza jambo Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan wakati wa mkutano huo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akieleza namna Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China inavyofanya kazi leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha pamoja kilichowahusisha Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na China. Wengine  ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila.  
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman.
  Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa.
 Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akimweleza jambo jaji wa Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya kumkaribisha Ofisini kwake Mahakama Kuu leo jijini Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akiwa katika mazungumzo na Jaji wa Mahakama Kuu ya China na baadhi ya Majaji kutoka  Mahakama hiyo waliomtembelea Ofisini kwake Mahakama Kuu jijini Dar es salaam.
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (wa pili kutoka kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (katikati) na baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Tanzania mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang ( kushoto) akiagana na  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (kulia) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi- Mahakama ya Tanzania
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu Nchini China Mheshimiwa Zhang Jiannan yuko Nchini kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi za Tanzania na China.
Katika ziara yake Nchini, Mheshimiwa Jiannan ambaye anamwakilisha Jaji Mkuu wa China, leo alikutana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa Mahakama zao.
Akizungumzia changamoto za Mahakama nchini China, Mheshimiwa Jiannan alisema hivi sasa Mahakama za China zinakabiliwa na upungufu wa Majaji ikilinganishwa na idadi ya kesi zinazosajiliwa.
Kwa Upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania alisema baadhi ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania ni pamoja na upungufu wa Mahakama za mwanzo.
Alisema ili kukabiliana na upungufu huo, Tanzania inahitaji kuwa na Mahakama za Mwanzo 3000 nchi nzima. Hivi sasa kuna Mahakama za Mwanzo karibu 960 nchini kote ambazo hazitoshi ikilinganishwa na Idadi ya kata zilizopo Nnchi mzima.Jaji Mkuu wa Tanzania alimshukuru Jaji Mkuu Kiongozi wa China kwa kuitembele Mahakama ya Tanzania.
Katika ziara yake nchini, Jaji Jiannan ameongoza ujumbe wa Majaji na Watendaji wengine wa Mahakama wanne kutoka nchini China.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU