MAGUFULI ATINGA GHAFLA BENKI YA CRDB DAR

RAIS Dk.John Magufuli leo ametinga a tawi la Benki ya CRDB Holland, Mtaa wa Samora na Ohio Dar es Salaam, akiwa kwenye gari binafsi bila kuwa na bendera ya rais wala nembo ya Taifa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio lililochukua dakika 25 lilitokea saa nne asubuhi likiwaacha watu vinywa wazi.

Dk.Magufuli ambaye siku ya pili tangu alipoapishwa alitembea kwa miguu hadi Wizara ya Fedha, jana baada ya kufika eneo hilo aliteremka kwenye gari na kuingia ndani ya benki hiyo, hali iliyosababisha baadhi ya wateja waliokuwa wakijiandaa kuingia kuzuiwa nje kwa muda kumpisha rais.

Baadhi ya wateja walielezea kushangazwa na tukio hilo, ambapo walisema ni historia kwani hawajawahi kuona rais akiingia katika tawi la benki kama wananchi wa kawaida.

Dereva wa taksi wa eneo hilo, Charles John alisema walishtuka baada ya kuona ulinzi ukiimarishwa ghafla eneo hilo na kujiuliza maswali mengi kabla ya Dk.Magufuli kuwasili.

"Tulidhani anakwenda Wizara ya Miundombinu kwenye ofisi yake ya zamani, kumbe akaingia CRDB," alisema.

Naye Joyce John aliyekuwa ndani ya benki hiyo wakati Rais Magufuli alipoingia alisema:"Nilikuwa ndani kwenye foleni kusubiri huduma, nikashtuka kuona rais ameingia."

Alisema baada ya rais kumaliza kilichompeleka alitoka na kwenda kwenye gari lake na kisha kuanza kupungia mkono wananchi waliokuwa wakimwangalia wakati akiondoka.

Habari, Picha kwa hisani ya Habari Mseto Blog

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

ZAKIA MEGHJI AWATIA HAMASA GIRL GUIDES, ATAKA WAWE JASIRI

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)