MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO KWA JESHI LA POLISI, CHUO CHA POLISI ZANZIBAR.

se1
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akipokea salamu ya heshima kwa Maafisa na wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
se2
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akikagua kwaride rasmin aliloandaliwa na Jeshi la Polisi alipofika kufunga mafunzo ya ungozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
se3
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akimvisha  cheo mmoja waaskari waliofanya vizuri zaidi G.944 Makuza Azekiel Shuka kwa niaba ya wenzake katika sherehe ya kumaliza mafunzo ya uongozi mdogo kwa ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti yaliyofanyika Chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
se4
Maafisa na wahitimu wa uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi wakitoa saluti kwa mgeni rasmini Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali.
se5
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika viwanja vya Jeshi hilo Ziwani Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Habari Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Khadija Khamis /Maryam Kidiko –Maelezo Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wahitimu  wa mafunzo ya uongozi mdogo kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuleta mageuzi makubwa ya utendaji katika sehemu zao za kazi.
Balozi Seif ameeleza  hayo leo katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Polisi  ngazi ya koplo, sajenti na staff sajenti yaliyofanyika katika viwanja nya Polisi Ziwani mjini Zanzibar.
Amesema kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wa kazi  itapelekea kupunguza uhalifu  na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Nategemea mtabadilika na kuwa watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi zitaendeshwa kwa haraka , haki itatendeka katika kutekeleza majukumu na haki za binaadam zitazingatiwa kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali na kuleta uhusiano wa karibu baina yenu na Wananchi “Alisema Balozi.
Aidha alilitaka Jeshi la polisi kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu huo hatimae hupelekea uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi.
Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame amewakumbusha wahitimu hao kuwa wanawajibu mkubwa wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na kulinda sheria za nchi.
Hata hivyo amewataka kufanya kazi kwa kutumia elimu waliyoipata chuoni kwa vitendo, kuwaelimisha na kuwaongoza kwa uweledi askari huko vituoni mwao.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa chuo cha Polisi Zanzibar Deusdedit Kaizilege Nsimeki amesema Jeshi la polisi litaendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi ili kuwajengea uwezo na uwelewa wa umuhimu wa utii wa sheria bila ya kushurutishwa.
Mafunzo ya uongozi mdogo wa vyeo vya Koplo, Sajenti na Staff sajenti yalifunguliwa rasmi tarehe 16/02/2016. Yakiwa na jumla ya wanafunzi 1532 kati ya hao kozi ya koplo 591, kozi ya Sajenti 706 na kozi ya Staff sajenti 235.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI