MKURUGENZI TAKUKURU ATINGA BUNGENI KWA ULINZI MKALI

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola akiingia bungeni Dodoma jana, huku akiwa na ulinzi mkali. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Takukuru, Kuruthum Mansoor. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Walinzi watano wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola wakiondoka kwenda kupumzika baada ya kuzuiwa lango kuu na Ofisa wa Bunge walipotaka  kuingia na Mlowola bungeni mjini Dodoma

 Baadhi ya walinzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola wakilinda wakati akipanda gari baada ya kuhudhuria kikao cha Bunge  mjini Dodoma jana, wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya ofisi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.



Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola ametinga leo bungeni mjini Dodoma huku akiwa na ulinzi mkali.

Kamshina Mlowola, alipoteremka kwenye gari lake alilakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Anjelah Kairuki na hatimaye kuingia bungeni asindikizwa na walinzi wapatao watano.

Waliokuwa wakimlinda Kamishna Mlowola walizuiwa  na Ofisa wa Bunge kuingia  lango kuu walipotaka kwenda na bosi wao ndani ya bunge. Walielekezwa eneo la kupumzika mpaka atakapotoka Mlowola.

Walinzi hao walitii amri ya ofisa huyo na kuondoka kwenda eneo waliloelekezwa kwenda kupumzika.

Kamishna Mlowola ambaye aliambatana na baacdhi ya maofisa akiwemo  Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Takukuru, Kuruthum Mansoor. Msafara wake ulikuwa wa magari mawili yenye rangi nyeusi.

Ndani ya Bunge Kamishna Mlowola na maofisa wake walikaa neo la wageni na baadaye kutambulishwa na Naibu Spika wa Bunge, Ackson Tulia kuwa ni wageni wa Waziri wa Nnchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Anjelah Kairuki ambaye siku hiyo ilikuwa zamu yake kusaoma bajeti ya ofisi hiyo. Takukuru ipo chini ya ofisi hiyo.

Kamishna Mlowola alipotoka nje kwa mapumziko alikutana na baadhi ya wabunge na kuteta nao ambao ni Mbunge wa Muheza, Adadi Rajab na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge.

Wakati anateta na wabunge hao mara walinzi wake walifika na kuimarisha ulinzi na hatimaye kuondoka na msafara wake.

Hivi karibu wabunge kadhaa wamefikishwa mahakamani na Takukuru kwa mashitaka ya Rushwa. Wabunge hao ni Richard Ndassa (Sumve), Kangi Ligora (Mwibara) na Sadick Muradi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU