MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATOA SIKU 6, OMBAOMBA WAONDOKE JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza kuhusiana na kuaza operesheni ya kuwaondoa ombaomba waliokandokando ya barabara, jijini Dar es Salaam leo. 
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa agizo la kuwaondo watu wanao ombaomba kandokando ya barabara jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi Blog)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa katika kuweka jiji hilo safi imejipanga kuanza na  mambo matatu ambayo ni kuwaondoa ombaomba wa barabarani, kuwabana wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na kuwaamuru  wamiliki wa bar kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba walikuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.

Makonda  ametoa siku sita mpaka April 18 ombaomba ndani ya jiji la  Dar es salaam wawe wameondoka
Kuhusu wamiliki wa Bar, Makonda  amesema wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.


Amesema mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini hiyo atailipa mwenyewe. 

Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari walipe faini na kuweka utaratibu  wa kupaki wapi magari yao au kubomoa majengo yao.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS