Mwana wa Besigye ashinda urais Oxford


AnslemImage copyrightFacebook
Image captionAnslem alitayarisha video ya kuwaomba wanafunzi wenzake wampigie kura
Mwana wa kiume wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye amechaguliwa kuwa rais wa chama cha mijadala chuo kikuu cha Oxford.
Anslem Besigye alikuwa ametengeneza video fupi ya kuomba wanafunzi wenzake wampigie kura.
Mamake Winnie Byanyima amefurahia ushindi wa mwanawe na kuandika kwenye Twitter: “Ameshinda! Anslem amechaguliwa rais wa chama cha mijadala katika bewa lake. Najionea fahari kama mamake.”
Kwenye video aliyokuwa ameitengeneza alikuwa amesimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.
Mwisho wa video mamake Bi Byanyima, alionekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.
Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*