NAPE:NITARUDISHA HESHIMA YA TASNIA YA HABARI NCHINI.

P3Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia  vitendea kazi  maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.
P2   Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na watumishi wa serikali wa mkoa wa Mara leo hii wakati wa Ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye mkoani humo.P5Kaimu Mkuu wa mkoa wa shinyanga Bi.Josephine Matiro akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye baada ya kuwasili mkoani hapo ili kujua changamoto mbalimbali za watumishi walio chini ya wizara yake na kuongea na wadau wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
P4Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo mwandamizi wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bw.John Igomego jinsi mitambo yakurushia matangazo ya shirika hilo inavyofanya kazi mkoa wa Mara.
P1Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza  na katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) mkoani Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe(mwenye kofia ya njano) kuhusu maendelezo ya uwanja wa kambarage ambao unamilikiwa na chama hicho mkoani hapo.Mhe.Nape amewaasa viongozi wa mkoa huo kutafta wadhamini ili kuuboresha uwanja huo.
……………………………………………………………………………………
Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema  kuwa atahakikisha heshima ya tasnia ya habari inarudi  baada ya kupitishwa kwa  mswada wa sheria ya huduma za vyombo vya Habari.
Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na Shinyanga na kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara hiyo na kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia  vitendea kazi  maafisa mawasiliano wa mikoa hiyo.
“Ule mswada utatoa tafsiri ya mwandishi wa habari,maana mwandishi wa habari lazma awe na sifa.Siku hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi alafu akajifunza kupiga picha akajiita na yeye mwandishi wa Habari.Ukifanya ivyo tasnia hii inakosa heshima,kwaiyo sheria ile itatafsiri nani mwandishi wa habari”Alisema Nape.
Aidha Waziri Nape alisema kuwa kwa kufanya hivi sheria hii itatibu tatizo la kulipwa vibaya na wamiliki wa vyombo vya habari maana mwandishi huyu atakuwa na elimu,maana kama hana elimu mmiliki ataajili mtu anaejua kusema wa kijuweni alafu ndo anamuajiri anakuwa mtangazaji  wa radio yake kisa tu anajua kusema.
Pamoja na hayo waziri uyo mwenye dhamana ya wizara nyeti ya habari alisema kuwa sheria hiyo pia itazungumzia maslahi ya mwandishi wa habari,itawabana wamiliki na mswada huu ukipita utarudisha heshima ya tasnia hii ya habari katika nchi yetu.
Akizungumzia upande wa radio kujenga nchi waziri nape amewaasa waandishi wa habari na watangazaji wa radio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha watanzania  kupitia radio zao  na si kuwatenganisha akitolea mfano wa yaliyotokea nchini Rwanda kwamba radio zilitumika kuhamasisha mauaji.
Mheshimiwa Nape pia amehaidi kuimarisha vitengo vya mawasiliano  serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapa maafisa hao vitendea kazi, pia ameliomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa na amehaidi kuzungumza na jeshi hilo ili waandishi hawa waweze kupata taarifa kirahisi.
Waziri uyo yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera,Mara,Shinyanga,Tabora na Singida ikiwa na lengo kuu la kuileta Wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na Michezo mikoani na wilayani karibu na wadau.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.