Kamishna Thobias Andengenye kushoto (PICHA YA MAKATABA)
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi
Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25
Aprili, 2016.
Kamishna wa Polisi
Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha
ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi
huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na
Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.
Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.
Uteuzi wa Dkt.
Donan Mmbando umeanza tarehe 24 Aprili, 2016.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
25 Aprili,
2016
Comments