RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA ASKOFU MATHIAS ISSUJA



ASKOFU AFARIKI: Askofu msaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mathias Issuja amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mt. Gaspar, Itigi, Dodoma.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Askofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Mathias Issuja Joseph, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Aprili, 2016 Mkoani Singida.

Baba Askofu Mstaafu Mathias Issuja aliyekuwa na umri wa miaka 87, amekutwa na mauti katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspar iliyopo Itigi, wilaya ya Manyoni Mkoani Singida alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema Askofu Mstaafu Mathias Issuja alikuwa Mzalendo wa kweli, kipenzi cha watu, aliyefanya kazi kubwa ya kuwajenga watu kiroho na kimwili, na kamwe mchango wake katika maendeleo ya Elimu, Afya na malezi ya watoto yatima hautasahaulika.

"Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Baba Askofu Mathias Issuja. Kazi kubwa aliyoifanya duniani kuwahudumia watu kiroho na kimwili ni vigumu kuipima, nitamkumbuka daima" Amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amemuomba Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, kufikisha pole nyingi kwa baraza la Maaskofu, Waumini wa Kanisa Katoliki na wote walioguswa na msiba huo na amemuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Aprili, 2016

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA