WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI CHALINZE WANUSURIKA KIFO CHA MOTO

moto2
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete alipokwenda jana kutembelea shule ya sekondari Chalinze baada ya bweni la wanafunzi wa kiume kuungua kutokana na shoti ya umeme. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
motoBweni lililoongua kwa shoti ya  umeme jana.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
WANAFUNZI   65 wa shule ya sekondari chalinz e iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamenusurika kifo baada ya bweni lao  kuteketea kwa moto wakati wao wakiwa darasani kwa ajili ya kujisomea masomo ya usiku.
Akizungumza na MWANDISHI WA HABARI HIZI kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema tukio hilo limetokea april 17 majira ya saa 3:20 usiku .
Mkuu huyo alisema chanzo cha moto huo inadaiwa ni shoti ya umeme ambayo imesababisha moto huo kuteketeza vifaa vyote vikiwemo magodoro,vitanda,vitabu katika bweni hilo.
Mwanga akizungumzia kuhusiana na juhudi za serikali ambazo tayari wameshazichukua hadi sasa alisema wanawahifadhi wanafunzi hao  katika jengo lingine la muda ambalo lilikuwa linatumika kwa chakula.
Alisema kuwa pia serikali ya mkoa imeshaanza kuwasiliana na wadau mbalimbali ambao watasaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa kusaidiana na serikali ili kujenga bweni jingine.
“Siwezi kusema hali ni nzuri kutokana na watoto wameunguliwa vifaa vyao,ni hasara katika jengo  pia kwahyo kilichopo sasa ni kumshukuru mungu kwa wanafunzi hawa kunusurika”alisema Mwanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Chalinze Hussein Mramba alikiri kutokea kwa tukio hilo 
Alisema mkandarasi wa halmashauri ya wilaya hiyo bado anaendelea na tathmini ya miundombinu iliyoungua.
Shule ya sekondari Chalinze ina jumla ya idadi ya  wanafunzi 1,151 kati yao 65 kwa sasa wameunguliwa na vitu vyao vyote hivyo kunahitajika juhudi za jamii,wadau na serikali katika kuhakikisha wanatoa msaada wa hali na mali .
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.