WANANCHI WA JIMBO LA HANDENI WAMLILIA WAZIRI WA MAJI
WAZIRI  wa maji Mhandisi  Gerson Lwenge pichani )kushoto ameombwa  kuingilia kati  na  kushughulikia  kwa haraka  utata  uliogubika  utekelezaji  wa mradi  wa  Bwawa  la maji  la malezi  lilipo kata  ya Malezi ,Mjini Handeni  ambao  haujaanza  licha  ya Benk ya Dunia  kutoa shs. 740  kwa  ajili  ya mradi huo.
Wakizungumza katika mahojiano na wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo, wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia maji  katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni sababau ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo kutolewa.
Kitombo alisema kwa taarifa alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo ambao  unatarajiwa  uwanufaishe Wakazi Zaidi  ya 6000. Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880.
Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha zilizoingizwa kaikamakauntinkuwa shs. Milioni 700
Pia alieleza mshangao wake kwa nini mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.

(Pichani kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini,Omari Kigoda)
Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyoya Malezi. Muhaji Ramadhani Mlaki alisema kuwa mara nyingi ammepokea wataalamu ambao wanakuja kuona eneo lakini hakuna kinachoendelea baada ya hapo licha ya kuwaambia watu wenye maeneo yao ambayo yameingizw kwenye mradi huo waache kulima.
“Tunapata lawama kwa wananchi kwa sababu tunawalewesha hadi mwisho wanatuambia kuwa na sisi tumekuwa wanasiasa,” alisema.
 Naye Cecilia Ibrahimu wa Malezi Kwedinguzo ambaye ana shamba kwenye eneo hilo la mradi wa bwawa alikubali kutoa eneo lake kwa sababu maji ni kero inayowagusa watu wote.
“Sina cha kusema nataka maji tu. Cha ajabu tuliambiwa tutapewa mashamba na kusaidiwa kulimiwa lakini mpaka sasa hatujaonyeshwa mashamba na mradi haujaanza,’ alisema Bi. Cecilia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata hiyo, Mzee Abdallah Kombo walipoingia katika uongozi kilio ni hicho hicho hadi hivi sasa. Alisema kuwa wananchi wanategemea malambo madogo yaliyochimbwa kwa juhudi za Mbunge wa zamani wa Handeni, marehemu Abdallah Kigoda.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS