WANANCHI WA KIJIJI CHA MANG'OLA WILAYANI KARATU WAIOMBA SERIKALI KULIFUNGUA ZIWA EYASI




Na Woinde Shizza,Karatu

Wananchi wa kijiji cha Malekichanda kilichopo katika kata ya Mang’ola wilayani karatu mkoani Arusha wameiomba Serikali kulifungua ziwa Eyasi ili waweze kufanya shughuli zetu za kimaendeleo na kujikwamua katika suala zima la umaskini.

Serikali imelifungia ziwa hilo,hali inayowapelekea vijana wengi kutojishughulisha katika shughuli zao mbalimbali za ujenzi wa Taifa ikiwemo pia suala la Kilimo na uvuvi,kwa sasa hali imekuwa ngumu,vijana wengi hawajishughulishi na uvuvi tena,aidha hali hiyo inaweza kusababisha wananchi wa eneo hilo kukumbwa na baa la njaa kutokana na kumaliza chakula chote ambacho walikuwa wamekihifadhii kwa ajili ya chakula cha akiba.

Hayo waliyasema jana wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipofanya ziara yakutembela na kukagua baadhi ya miradi inayofanywa na chama pamoja na kuongea na wananchi wa kata hiyo.

Walisema kuwa wanasikitishwa sana na kitendo cha mkuu wa wa Wilaya kuwasimamisha shughuli zao za uvuvi ,kwani ndizo walizokuwa wakizitegemea katika kujipatia kipato pamoja na chakula katika kijiji hicho na kata kwa ujumla.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Kristopher Nyato alisema kuwa tangu machi 19 walizuiwa kufanya shughuli zao za uvuvi katika eneo hilo na kupewa masaa 24 kuondoka katika eneo hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa eneo hilo limekubwa na ugonjwa wa kipindu pindu.


Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anajaza mchanga kwa ajili ya kufetua matofali hiii ikiwa nimoja ya mradi ambao ameutembelea katika kata hiyo.
Diwani wakata ya mang'ola Lazaro Gege akiwa anampa maelezo kwa ufupi ya mradi wa matofali kaimu katibu mkuu wa vijana CCM taifa.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm Mkoa Arusha Sabaya Lengai akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hii leo wakati wa ziara ya kaimu katibu mkuu wa vijana taifa.
baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kufatilia mkutano huo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.