WANANCHI WA USHIRIKA TUKUYU WAZUILIWA KUJENGA ZAHANATI


1Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi hao ambao waliomzunguka kutoa kero yao ya kuzuiwa kuendelea na ujenzi wa zahanati.
4Wananchi wa kata ya Ushirika-Tukuyu wakiwa wamebeba bango kuonesha kilio chao kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto.
23Mmoja wa mwanakamati akimueleza mgogoro wao wa eneo la ujenzi wa zahanati kati yao na mkurugenzi wa halmashauri yao.
………………………………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura
Wananchi wa kata ya ushirika wilayani tukuyu wameusimamisha msafara wa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto uliokua ukitoka wilayani kyela kuelekea mbarali kwa madai hawana kituo cha afya wala zahanati kwa miaka hamsini sasa.
Wananchi hao ambao walikua wameshika bango kubwa lililoandika hawamtaki mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa madai ya kuwasimamisha ujenzi mara mbili
Akieleza kilio chao katibu.wa kamati ya ujenzi  bi.fatma mwandegele alisema eneo hilo limeingia kwenye mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu kati ya kijiji cha mpunguso na aliyekua katibu tarafa wa kata ya pakati bw.mwakapala
Hatahivyo alisema kesi kuhusu eneo hilo ilishamalizika na wananchi walikusanya nguvu zao kwa kuchangia simenti na mawe hata hivyo simenti hiyo iliharibika
Waziri Ummy Mwalimu ilimrazimu kwenda kuliona eneo hilo ambalo  limechimbwa tayari kwa kuanza msingi huku mawe yakiwa yamerundikwa pasipo kuendelea na ujenzi alimuagiza mganga mkuu wa mkoa ambaye alikua nae kwenye msafara wake,siku ya jumatatu wafike eneo hilo pamoja na mkurugenzi na mganga mkuu wa wilaya ili waeleze kwanini wasiendelee na ujenzi wa zahanati hiyo.
“Nawaomba wananchi muwe watulivu ili tujihakikishie kama kesi hiyo imekwisha na kwanini tusiendelee na ujenzi huu na jumatatu kabla ya.saa tisa mchana niwe nimepata ripoti ya eneo hili
Aidha,Waziri huyo aliwathibitishia wananchi hao kwamba lazima zahanati ijengwe kwenye kijiji hicho ili kiweze kuwahudumia wananchi na kuwaahidi.serikali itawaletea wahudumu pamoja na dawa,vifaa na vifaa tiba.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)

WAGGGS AFRIKA WAIPONGEZA TGGA KWA KUONGOZA AFRIKA KUSAJILI GIRL GUIDES WENGI