WASHTAKIWA WA TUMBILI WASOTEA DHAMANA.


Baadhi ya Washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi ya usafirishaji wa
wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa
wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem
Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi
kuingia mahakamani,Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem
Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi ,kulia ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt Charles Mulokozi.
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili wakiwa katika mahabusu ya
mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, kutoka kulia ni Eduard Vardanyan ,ArtemVardanian na Idd Misanya.
Watuhumiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili wakiwa katika mahabusu ya
mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, wakizungumza jambo na wakili
Majura Magafu anyewatetea katika shauri hilo.kutoka kulia aliyeshika
nondo ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Wanamapori Dkt Charles
Mulokozi, mfanyabiashara raia wa Uholanzi Artem Vardanian na ndugu yake
Eduard Vadanyan.
 …………………………………………………………
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
 
HATMA ya dhamana kwa washtakiwa saba wa makosa ya uhujumu uchumi wakiwamo wafanyabiashara raia wa
Uholanzi waliokamatwa Machi 23 mwaka huu wakijaribu kusafirisha wanyama hai 61
aina ya Tumbili sasa kujulikana Alhamisi (Aprili 14).
Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi ,Aishiel
Sumari wakati akitoa uamuzi mdogo juu ya hoja zilizotolewa na upande wa utetezi
ukiongozwa na wakili Majura Magafu dhidi ya upande wa Jamhuri kuhusu maombi ya
dhamana kwa washtakiwa.
Hoja za upande wa utetezi zilitokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha mahakamani hapo hati zuio
la dhamana kwa washtakiwa wote saba iliyotoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini
(DPP).
Maombi matatu ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo ambayo ni ombi la tatu la  raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian ,Eduard
Vardanyan na Idd Misanya ,ombi nne la 
,Nyangabo Musika,Martina Nyakanga na
Very Anthon huku ombi la tano lilikuwa ni la aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa
idara ya wanyamapori nchini Dkt Charles Mulokozi.
Baada ya maombi hayo kuwasilishwa upande wa utetezi uliridhia kuunganishwa kwa maombi hayo ili kuokoa muda wa mahakama katika kusikiliza shauri hilo baada ya maombi hayo kufanana.
Akitoa uamuzi huo Jaji Sumari aliuelekeza upande wa jamhuri kupitia kwa wanasheria wa Serikali
Wankyo Simon na Robart Rogart kutumia siku ya leo (Jumanne) kuwasilisha hoja
kinzani na kwamba upande wa utetezi utawasilisha maombi yao kesho (Jumatano)  baada ya kujibiwa na upande wa pili.
Awali akiwasilisha hoja za upande wa utetezi kwa niaba ya mawakili wenzake ,Wakili Majura Magafu alieleza
kuwa na pingamizi juu ya upokelewaji wa hati ya zuio la dhamana kwa washtakiwa
hao na kwamba imewasilishwa kabla ya maombi ya dhamana ya washtakiwa hao  hayajaunganishwa.
“Ni mtazamo wetu kwamba uwasilishwaji wa hati ya zuio la dhamana ulipaswa kufanyika kabla ya
kuunganishwa kwa maombi ya dhamana  ,certificate
(hati ya dhamana)  iliyo mbele ya
mahakama sio Proper kuwepo”alieleza Magafu.
Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na mwanasheria wa serikali Wankyo Simon huku akieleza mahakama
kuwa upande wa utetezi unajaribu kuipotosha mahakama bila ya kutaja kifungu cha
sheria kinachoonesha makosa yaliyopo.
Washtakiwa wote saba wamerudishwa rumande hadi Aprili 14 ambapo shauri hilo namba 1/2016
litakapofika mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji .
Washitakiwa katika shauri hilo ni Dk.Charles Mulokozi mkurugenzi
msaidizi wa wanayamapori,Nyangabo Musika ambaye ni Ofisa mfawidhi anayehusika
na matumizi endelevu ya wanyamapori nchini(Cites),Martina Nyakanga ambye ni
kaimu mkuu wa kanda kikosi cha KDU Arusha.
Wengine ni ofisa wanyamapori Arusha,Very Gelard Anthony,Idd Misanya
mmiliki wa Kampuni ya Birds Traders ya JIjini Arusha  na raia wawili wa
uholanzi,Artem Vardanian na Eduard Alik Vadanyan ambaye ni meneja wa Hotel ya
North Sea.
Raia hao wawili wa Uholanzi walikamatwa machi 23 mwaka huu katika uwanja
wa ndege  wa Kimataifa  wa Kilimanjaro(KIA) wakijiandaa kusafrisha
wanyama hai 61 aina ya tumbili kwenda nchini Armenia wanaodaiwa kuwa na thamani
ya dola za kimarekani 7,320 zaidi ya sh,Milioni 15 .
Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza April mosi
mwaka huu mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mkoa,Joachim Tiganga na
kusomewa mashitaka matatu likiwamo la uhujumu uchumi,kula njama na kusafrisha
wanyama hai.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka,washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya
februari mosi ya machi 22 katika miji ya Arusha,Kilimanjaro na Dar es
salaam,washitakiwa walikula njama  kwa nia ya kutenda kosa la kusafrisha
nyara za serikali .
Mawakili wa serikali ,Wankyo Simon na Salim Msemo wakiongozwa na wakili
mwandamizi Abdallah Chavula,walidai katika shitaka la pili kuwa,mnamo machi 23
mwaka huu washitakiwa hao walikula njama za kusafrisha wanyama hai .
Pia washitakiwa Artem Vardanian na Eduard Alik Vadanyan ambao ni raia wa
kigeni,pia wanashitakiwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya ununuzi na
usafrishaji wa wanyama hai kwenda nchini Armenia bila kuwa na kibali cha
mkurugenzi wa wanyama pori.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.