WAZEE WA ZANZIBAR WAANZA KUPOKEA PENSHENI

pe1
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na watu wenye ulemavu wa Tanzania Bara Dk. Abdallah Possi  alipofika katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
pe3
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na watoto Moudline Castico akielezea mikakati yao yakuwasaidia wazee katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa Wazee wa Zanzibar (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed.
pe4
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni ya Sh/= elfu 20 Mzee. Kombo Moh’d Kombo itakayokuwa ikitolewa kila mwezi, katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
pe5
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni Bi. Erestina Filex katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa leo April 15/2016.
pe6
Baadhi ya Wazee waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
………………………………………………………………………………………………………………
Na Miza Kona, Majda  Kasim -Maelezo Zanzibar.
Wazee 21,750 wameanza kunufaika na mpango wa serikali wa utoaji fedha za kujikimu yaani pensheni kwa wazee wote wanaoanzia umri wa miaka 70 ili kuimarisha maisha yao.
Wazee 13,150 ni kutoka Unguja na 8,600 wanatoka Pemba, katika mpango huo, kila mzee atapewa shilingi elfu ishirini kila mwisho wa mwezi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, katibu mkuu wizara ya uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto Asha Ali Abdallah, amesema hatua hiyo ni muhimu kwani nchi nyingi duniani zinao utaratibu kama huo.
Amesema, mbali ya kuwa kufanya hivyo ni wajibu, lakini kunahitaji maamuzi ya kijasiri na utashi wa kisiasa, ambapo serikali ya Zanzibar imeweza kuonesha dhamira yake kuimarisha maisha ya wazee.
Amesema msingi wa pensheni kwa wazee wote wa Zanzibar, ni sera ya hifadhi ya jamii iliyopitishwa mwaka 2014, ukiwa mpango mkuu wa taifa wa dira ya 2020 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umasikini nchini.
sambamba na hilo alisema kuwa wataendelea kuwa na jukumu kubwa katika kuwasajili wazee wapya watakaokuwa wanaingia katika mpango huo.
Waziri wa fedha Dk Khalid Salum Mohammed, alisema kuwa ili serikali iweze kupata maendeleo ni lazima wafanyakazi na wananchi kuwa wawajibikaji katika utendaji wa kazi zao.
Alisema katika kutekeleza mpango huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu na waaminifu ili kuhakikisha wazee wanaostahi wanapata pencheni zao kama inavyopaswa.
“hali halisi na uzoefu unaonesha kuwa kumekuwa na tabia za udanganyifu na wizi katika masuala mengi yanayohusiana na malipo….lakini nachukua nafasii hii kuwatanabahisha watendaji wote watakaohusika na utekelezaji wa mpango huu katika ngazi zote yoyote atakaebanika kufanya udanganyifu hatua kali zinatuchukuliwa dhidi yake”alisema.
Aidha aliwataka watendaji wa mpango huo kuwa na hekima,busara,uvumilivu,upole na huruma ni lazima zichukue nafasi yake katika kuwahudumia wazee.
Nae waziri wa Kazi,uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Moudline Castico ameahidi kwamba mpango huo utasimamiwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha wazee wote wanaostahiki wanapatiwa fedha zao kwa wakati na hakutakuwa na udanganyifu na upotevu wa fedha za serikali.
Mpango huo unatarajiwa kutumia shilingi miioni 435 kwa mwezi ambapo ni sawa na shilingi bilioni 5.220 kwa mwaka.
Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza Afrika mashariki kuanzisha mpango huo, nay a sita kwa Afrika baada ya Mauritius, Afrika Kusini, Lesotho, Namibia na Botswana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA