YANGA YAIFUMUA MTIBWA, YATINGA KILELENI


Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 jioni ya leo dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, Simon Happygod Msuva na sasa Yanga SC inafikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi 24 na kuwateremshia nafasi ya pili mahasimu wao Simba wenye pointi 57 za mechi 24.
Hata hivyo, Simba wanaweza kurejea kileleni kesho wakiifunga Toto Africans kwenye Uwanja huo huo katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.
Msuva alifunga bao hilo dakika ya 47 kwa shuti la umbali wa mita 28 baada ya kuanzishiwa mpira wa adhabu ndogo na kiungo Haruna Niyonzima.
Simon Msuva ameirejesha Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu leo

Kipindi cha kwanza, kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm Pluijm alianzisha mabeki wa tatu wa kati kwa pamoja, Kevin Yondan, Vincent Bossou na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, huku akitumia mshambuliaji mmoja tu, Donald Ngoma.
Hali hiyo iliwafanya Yanga wasiwe na makali sana katika safu yao ya ushambuliaji, huku krosi nyingi za kutokea pembeni zikipitiliza au kuchezwa na mabeki wa Mtibwa. 
Lakini mabadiliko aliyoyafanya Pluijm anayesaidiwa na mzalendo, Juma Mwambusi mapema kipindi cha pili kumtoa beki mmoja wa akti, Yondan na kumuingiza mshambuliaji, Malimi Busungu yalirudisha makali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Simon Msuva (kushoto) akikimbilia mpira dhidi ya beki wa Mtibwa, Salum Mbonde
Simon Msuva akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Taifa 

Hata hivyo, safu ya ulinzi ya Mtibwa ikiongozwa na kipa wa zamani wa Yanga, Said Mohammed iliendelea kuwa imara na kutoruhusu mabao zaidi. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan/Malimi Busungu dk46, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke/Amissi Tambwe Dd73. 
Mtibwa Sugar: Said Mohamed, Ally Shomari, Majaliwa Shaaban, Andrew Vincent, Salim Mbonde/Boniface Maganga dk83, Shaaban Nditi, Shiza Kichuya/Vincent Barnabas Dd73, Muzamil Yassin, Ibrahim Rajab ‘Jeba’/Henry Joseph Shindika dk52, Suleiman Rajab na Kelvin Friday.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI