ZAHANATI YA KIJIJI CHA UTURO YATOKOMEZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI KWA MIAKA 18


Ummy Mwalimu
Na.Catherine Sungura, Mbarali
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,,ameipongeza zahanati ya uturo wilayani Mbarali kuwa ni ya mfano Tanzania kwa kuzuia vifo vitokanavyo na mama wajawazito  na watoto wachanga
Waziri Ummy ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipoenda kutembelea zahanati hiyo na kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana katika kuzuia vifo hivyo.
“Ninawapongeza sana wananchi wote wa Uturo kwa kazi kubwa na nzuri katika kudhibiti vifo vya watoto wachanga na akina mama,nataka kuwathibitishia zahanati ya uturo ni ya mfano kitaifa.
Alisema haikubaliki kwa mwanamke yeyote Mjamzito kufariki kwa sababu ya kutimiza haki yake ya kuzaliwa ya kuzaa,wanawake wameumbwa kuzaa,hivyo hakuna mtu atakayeweka vikwazo mwanamke asizae
“Kila mwanamke anayebeba ujauzito, mategemeo yake yeye na kichanga watakuwa hai na salama,hakuna mwanamke anayebeba ujauzito kwa mategemeo ya mtoto wake kufariki”
Aidha,alisema anautambua mchango mkubwa kwa watoa huduma ngazi ya jamii kwa kufuatilia wanawake wote wajawazito kuhudhuria kliniki kipindi chote cha ujauzito  pamoja n jamii yote kuwajibika na kushiriki katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi
“Popote nitakapoenda na kusimama
 kuzungumzia kupambana na vifo vitokanavyo na vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga,nitatolea mfano zahanati hii.
Hata hivyo waziri Ummy alisema Moja ya kipaumbele chake katika wizara hii nikupunguza vifo vya mama wajawazito watoto wachanga
Katika pongezi hizo waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto hakusita kuwapongeza wanaume wote kwa kuwa jeshi la kupambana na vifo hivyo”wanaume wote wa vitongoji vya ukwama,ukwishikiro,mtamba na ukwaviro asanteni sana ninyi ni wanaume bomba kwa kuwajali wenza wenu na watoto.
Awali mganga mfawidhi wa zahanati hiyo Wilison Chotamganga alisema jitihada za kutokomeza vifo hivyo vilianza mwaka 1998 mara alipohamishiwa kijijini hapo na kukuta matuta (makaburi)madogo mengi hivyo akaamua kuunda uongozi wa watu watano kwa kila kitongoji na kuweka mikakati ya kuzuia akina mama kujifungulia nyumbani na kila mwanaume na mwenza wake wanahudhuria kliniki kuanzia ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa takwimu za tanzania zinaonesha kila saa moja mwanamke mmoja anafariki wakati wa kujifungua,hivyo kwa siku wanawake ishirini na nne wanafariki,720 kwa mwezi na takribani wanawake 8,600 wanafariki kwa mwaka

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*