China yakana kuuza nyama ya binaadamu Afrika



Image captionNyama ya mkebe kutoka nchini China
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng'ombe.
Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.
Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.
Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.
Image captionNyama ya mkebe kutoka China
Balozi wa China nchini Zambia,Yang Youming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili.
''Leo jarida moja linasambaza uvumi ,likidai China inatumia nyama ya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika.
''Hii ni dhulma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi''.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA